James Mattis alikuwa waziri wa ulinzi wa kwanza wa Rais Trump - ila alijiuzulu mwaka 2018 |
Alisema “alikuwa na hasira na kushangazwa” ya namna Bw Trump alivyokuwa akishughulikia maandamano yanayoendelea juu ya kifo cha Mmarekani mweusi George Floyd mikononi mwa polisi.
Bw Mattis amekosoa vikali “utumiaji mbaya madaraka” ya Bw Trump na kuwaunga mkono waandamanaji wanaotaka kuhakikisha maadili ya Marekani yanazingatiwa, kama ilivyokuwa kwa Rais mstaafu Barack Obama.
Bw Trump amemwelezea Bw Mattis kama “jenerali anayekuzwa kuliko anavyostahili”
Bw Mattis aliachia ngazi mwaka 2018 baada ya Bw Trump kuamua kuondosha majeshi ya Marekani nchini Syria.
Alikuwa kimya muda wote mpaka alipoamua kumtolea uvivu Bw Trump kupitia jarida la Atlantic.
Katika kujibu mashambulio, Bw Trump aliandika mfululizo wa ujumbe kupitia ukurasa wake wa twitter akidai kuwa alimfukuza kazi Bw Mattis.
"Sikupenda “uongozi wake” mtindo wake au hata yeye mwenyewe, na wengi wanakubaliana na hilo," aliandika. "Nashkuru aliondoka!"
Chanzo:BBC
No comments:
Post a Comment