Thursday 2 April 2015

KATIBA MPYA TZ: HAKUNA KURA YA MAONI APRILI 30

Mwenyekiti wa Nec Jaji Mstaafu Damian Lubuva

Tume ya Taifa ya Uchaguzi (Nec) imekubali kuahirisha upigiaji Kura ya Maoni ya Katiba Inayopendekezwa iliyopangwa kufanyika Aprili 30, mwaka huu kutokana na kutokamilika kwa uandikishaji wa Daftrai la kudumu la wapiga kura kwa kutumia teknolojia ya Biometric Voters Registration (BVR).

Hatua hiyo inakuja baada ya kuwepo mfululizo wa matamko na ushauri kutoka kwa wadau mbalimbali wa demokrasia kwamba zoezi hilo lisingewezekana kwa sasa hasa kutokana kusuasua kwa mwenendo wa BVR.

Mwenyekiti wa Nec Jaji Mstaafu Damian Lubuva aliwaambia waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo kuwa kazi ya uboreshaji daftari la wapiga kura ni ya msingi kabla ya taratibu zote za upigaji kura.

Jaji Lubuva aliyeonekana kuwa mpole zaidi, alisema kwa uzoefu walioupata Njombe, zoezi la uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura bado halijakamilika katika mkoa huo na mingine iliyosalia.

“Hivyo tume haitaweza kuendelea na zoezi la upigaji kura ya maoni na zoezi hilo lililotangazwa hapo awali kufanyika Aprili 30, 2015 limeahirishwa hadi tarehe itakapotangazwa na Nec baada ya kushauriana na Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar,” alisema Jaji Lubuva.

Kwa nyakati tofauti, vyama vya siasa, asasi za kiraia, taasisi za kidini na wananchi wamekuwa wakiishauri Nec kuahirisha Kura ya Maoni huku vyama vya siasa vikimtaka Rais Jakaya Kikwete atii makubaliano yaliyofikiwa na Kituo cha Demokrasia (TCD) mwaka jana ya kuahirisha zoezi hilo hadi baada ya Uchaguzi mkuu.

Jaji Lubuva alisema kuwa tume yake inaendelea kuboresha daftari la wapiga kura nchi nzima ambapo wanatarajia kukamilisha ifikapo Julai mwaka huu. Nec ilieleza kuwa baada ya kumaliza uandikishaji mkoani Njombe watahamia mikoa ya Ruvuma, Lindi, Mtwara na Iringa.

Chanzo: mwananchi.co.tz

SHAMBULIO LA CHUO KIKUU KENYA 'LAUA 147'



A Kenyan soldier escorts a woman after she was rescued

Idadi ya watu waliouawa katika shambulio lililofanywa na al-Shabab kwenye chuo kikuu kaskazini-mashariki mwa Kenya imeongezeka kufikia 147, maafisa wa serikali walisema.

Harakati za kijeshi za kudhibiti chuo kikuu cha Garissa sasa zimekwisha, huku washambuliaji wote wanne wakiwa wameuawa, walisema.

Maafisa walisema wanafunzi 587 walitolewa, 79 wakiwa wamejeruhiwa.

Sheria ya kupigwa marufuku kutoka usiku inatekelezwa katika baadhi ya sehemu nchini humo.

Kaunti nne katika mpaka wa Kenya-Somalia, Garissa, Wajir, Mandera na Tana River, wamezuia watu kutoka nje siku nzima.

Wanafunzi tisa waliojeruhiwa vibaya sana walisafirishwa kwa ndege kwenye mji mkuu Nairobi kwa matibabu.

Kwa maelezo zaidi, bonyeza link ifuatayo
http://bbc.in/1DrBXQW

CHUO KIKUU KENYA CHASHAMBULIWA



Map showing Garissa in Kenya

Watu wenye silaha waliovaa barakoa wamevamia chuo kikuu kimoja karibu na mpaka wa Somalia kaskazini-mashariki mwa Kenya, wakiua watu wawili na kujeruhi takriban 30.

Majeshi yamezunguka chuo kikuu cha Garissa na kujaribu kupambana na washambuliaji.

Walioshuhudia walizungumzia watu hao wenye silaha wakifyatua risasi ovyo bila kujali ni nani na hivyo kuhofiwa kuwa idadi ya waliokufa inaweza kuongezeka.

Haiko wazi nani anahusika na shambulio hilo, lakini wapiganaji wa al-Shabab wamekuwa wakiishambulia Kenya mara kwa mara.

Garissa na maeneo mengine ya mpakani yamekuwa yakishambuliwa mara nyingi.

Tuesday 31 March 2015

MUHAMMADU BUHARI ASHINDA NIGERIA



File photo: Goodluck Jonathan (left) and Muhammadu Buhari shake hands after signing a peace deal agreeing to respect the outcome of the polls
Goodluck Jonathan (kushoto) na Muhammadu Buhari walikubaliana wiki iliyopita kuheshimu matokeo ya uchaguzi

Aliyekuwa kiongozi wa kijeshi Muhammadu Buhari amekuwa mgombea wa kwanza wa upinzani kushinda uchaguzi wa urais Nigeria.

Chama cha Jenerali Buhari kimesema mpinzani wake, Goodluck Jonathan, alikubali kushindwa na kumpa pongezi.

Bw Jonathan alipishana na Jenerali Buhari kwa takriban kura milioni mbili alipogoma mara ya kwanza kukubali kushindwa.

Waangalizi kwa ujumla wameusifia uchaguzi lakini kumekuwa na madai ya udanganayifu, ambao baadhi wanahofia kunaweza kusababisha maandamano na ghasia.

Kwa taarifa zaidi, bonyeza link ifuatayo

http://www.bbc.co.uk/news/world-africa-32139858

BUHARI 'ANAONEKANA' KUONGOZA UCHAGUZI NIGERIA



People watch election news coverage on television at a street in Lagos, Nigeria, 30 March 2015

Matokeo ambayo bado hayajakamilika kutoka uchaguzi wa Nigeria unaashiria aliyekuwa kiongozi wa kijeshi Muhammadu Buhari amepata kura zaidi kuliko rais wa sasa aliye madarakani, Goodluck Jonathan.

Hata hivyo, majimbo yenye watu wengi zaidi kama vile Lagos na Rivers bado matokeo hayakutangazwa rasmi.

Huku nusu tu ya majimbo ya Nigeria yakiwa yametangazwa, chama cha Jenerali Buhari cha All Progressives Congress (APC) kiliripotiwa kuwa na kura zaidi kwa milioni mbili.

Matokeo zaidi yanatarajiwa kutangazwa siku ya Jumanne.

Tume ya uchaguzi ya Nigeria (Inec) ilisitisha kutangaza matokeo Jumatatu usiku, baada ya kutoa matokeo ya majimbo 18 na mji mkuu Abuja.

Chama cha Rais Jonathan cha People's Democratic Party (PDP) kilipata kura 6,488,210 na cha APC cha Jenerali Buhari kimepata kura 8,520,436.

                                                                                                                                                                                        

Monday 30 March 2015

MWENDESHA MASHTAKA WA UGANDA AUAWA



Security checks in Kampala, 26 March
Ulinzi uliimarishwa baada ya onyo la shambulio la ugaidi

Joan Kagezi, mwendesha mashtaka mkuu wa Uganda katika kesi ya watu 13 walioshutumiwa kwa shambulio kubwa la bomu la al-Shabab, amepigwa risasi na kufariki dunia mjini Kampala.

Bi Kagezi alilengwa na watu wenye silaha waliokuwa kwenye pikipiki alipokuwa njiani akielekea nyumbani.

Shambulio la bomu la kujitoa mhanga la mwaka 2010 Kampala lilisababisha vifo vya watu 76 walipokuwa wakitazama fainali ya Kombe la Dunia.

Wiki iliyopita, ubalozi wa Marekani Uganda iliwaonya raia wote wa kigeni – wakiwemo Wamarekani – uwezekano wa kulengwa na mashambulio ya “kigaidi” mjini Kampala.

Bi Kagezi, wakili mwandamizi, aliongoza idara ya umma ya kuzuia ugaidi na pia idara ya uhalifu wa kivita.

Msemaji wa polisi wa Kampala Patrick Onyango alisema: "Walikuwa wakimfuatilia na pikipiki – walimpiga risasi na kumwuua.