Monday 2 March 2015

BILL GATES, ATAJWA KUWA TAJIRI WA DUNIA TENA



Bill Gates
Bill Gates

Bill Gates ametangazwa kuwa mtu tajiri duniani kwa mara ya 16 na jarida la Forbes linalotoa orodha ya mabilionea wa dunia kila mwaka.

Muasisi wa Microsoft kwa mara nyingine tena amemshinda mfanyabiashara wa Mexico  Carlos Slimna na kuchukua nafasi ya juu.

Utajiri wa Bw Gates uliongezeka kwa zaidi ya dola bilioni 3 kwa mwaka hadi Februari 13, na kufikia dola bilioni 79.

Forbes imesema kuna rekodi ya mabilionea 1,826 duniani, ongezeko la wengine 181 katika kipindi cha miaka 12 iliyopita.

Bw Gates amekuwa nafasi ya kwanza mara 16 katika kipindi cha miaka 21, Forbes iliongeza.

Mwekezaji maarufu wa Marekani Warren Buffet amefanikiwa kurejesha nafasi yake ya tatu katika orodha hiyo akiwa na thamani ya dola bilioni 72.7, na kumzidi Amancio Ortega, mwanzilishi wa maduka ya ubunifu ya nguo Hispania yaitwayo Zara.

 

Matajiri 10 bora kulingana na Forbes 2015:

 
1. Bill Gates $79.2bn (Microsoft)

2. Carlos Slim Helu $77.1bn (Phones and construction in Mexico)

3. Warren Buffett $72.7bn (Global investor)

4. Amancio Ortega $64.5bn (Zara and other fashion chains)

5. Larry Ellison $54.3bn (Oracle data storage technology)

6. Charles Koch $42.9bn (Industrialist)

7. David Koch $42.9bn (Industrialist)

8. Christy Walton $41.7bn (Walmart retail giant)

9. Jim Walton $40.6bn (Walmart retail giant)

10. Liliane Bettencourt $40.1bn (L'Oreal cosmetics firm)





No comments:

Post a Comment