Tuesday 10 March 2015

MPINZANI WA BURUNDI ALITOKA GEREZANI 'KIULAINI'


Hussein Radjabu during his trial in April 2008
Hussein Radjabu
Mpinzani mkuu nchini Burundi Hussein Radjabu ameiambia BBC kuwa alitoroka kutoka gerezani wiki iliyopita kwa kutembea “bila wasiwasi wowote”.

Polisi wa Burundi walisema maafisa wa gerezani walimsaidia kutoroka.

Radjabu alisema sasa yupo na wafuasi wake – lakini hakueleza ni wapi hasa alipo.

Aliyekuwa mkuu wa chama hicho tawala alikuwa akionekana mwenye ushawishi mkubwa mno nchini Burundi mpaka alipokamatwa mwaka 2007, baada ya kuwepo na tetesi za kutoelewana na Rais Pierre Nkurunziza.

Pierre Nkurunziza

Aliphojiwa na BBC, Radjabu alimtuhumu rais kwa kupanga kufukuzwa kwake chamani, pamoja na kumwuundia kesi ya njama ya kupindua serikali.

Radjabu ametoroka baada ya kutumikia miaka minane kati ya 13 ya hukumu yake.

Alitoroka kwasababu ulikuwa "wakati muafaka kufanya hilo".

Kumekuwa na wasiwasi mkubwa unaoongezeka Burundi juu ya mipango ya rais kuongeza muhula wa tatu kuongoza nchini humo.

Hatua hiyo inakiuka katiba na makubaliano ya Arusha ya mwaka 2000, yaliyomaliza mapigano ya wenyewe kwa wenyewe yaliyodumu kwa miaka saba.

Inasemekana chama tawala cha CNDD-FDD kimegawanyika baina ya wale wanaomuunga mkono Bw Nkurunziza kuendelea kubaki madarakani, na wale wanaopinga.

Radjabu aliiambia BBC kuwa yeye bado ni mwenyekiti wa chama tawala na Rais Nkurunziza lazima alitambue hilo.

No comments:

Post a Comment