Muhammad limekuwa jina maarufu kwa watoto wa kiume nchini
Uingereza, mtandao wa BabyCentre umedai.
Wakati huohuo majina ya kiarabu yamezidi kutumika zaidi.
Vipindi vya televisheni kama vile Game of Thrones pia
vimechangia sana kutoa majina ya kizazi kijacho.
Orodha ya majina 100 bora ya watoto kwa mwaka 2014
imeonyesha Muhammad imepanda nafasi zaidi ya 27 kutoka mwaka jana hadi kufika
namba moja.
Jina hilo limepata nafasi hiyo baada ya kuchaguliwa na
watu 56,157 wa wanachama wa mtandao wa BabyCentre.co.uk waliojifungua mwaka
2014.
Kwa ujumla kumekuwa na ongezeko kubwa la majina ya
kiarabu, huku Nur likiwa jipya kuingia katika orodha hiyo katika majina 100
bora ya kike, likiruka hadi nafasi ya 29, na Maryam likipanda mara 59 na
kuchukua nafasi ya 35.
Omar, Ali na Ibrahim ni majina mapya kuingia katika 100
bora za kiume.
Sophia ndio namba moja katika majina ya watoto wa kike,
na kupata umaarufu tena katika orodha ya mtandao wa BabyCentre nchini Marekani,
Brazil, Hispania na Urusi mwaka jana.
Lakini jina linalotamba zaidi upande wa watoto wa kike ni
Maryam, huku majina mapya zaidi ni Nur, Emilia na Gracie.
Chanzo: www.theguardian.com
No comments:
Post a Comment