Thursday, 25 December 2014

BINTI ADAI WAZAZI WALIMKABIDHI KWA BOKO HARAM



Nigerian police present 13-year-old girl to reporters in Kano. 24 Dec 2014

Mtoto wa kike kutoka Nigeria mwenye umri wa miaka 13 ameelezea namna wazazi wake walipomkabidhi kwa wapiganaji wa Boko Haram ili ajitolee mhanga.

Binti huyo, akizungumza na waandishi wa habari iliyoandaliwa na polisi, alisema alipelekwa mjini Kano ambapo mabinti wengine wawili walilipua mabomu yao.

Takriban watu wanne walikufa katika shambulio la Desemba 10. Binti huyo alikamatwa, bado akiwa amevaa mabomu, polisi walisema.

Takriban watu 2,000 walikufa kutokana na mashambulio waliohusishwa nao wapiganaji hao mwaka huu.

Binti huyo aliwaambia waandishi wa habari kuwa wazazi wake walimpeleka kwa wapiganaji hao waliojificha msituni karibu na mji wa Gidan Zana katika jimbo ka Kano kaskazini mwa nchi hiyo.

Alisema mmoja wa viongozi wa kundi hilo alimwuuliza kama anajua maana ya kujitolea mhanga kutumia bomu.

"Walisema, 'Utaenda peponi ukifanya hivyo.' Nikasema 'Hapana siwezi.' Wakasema watanipiga risasi au kunirusha kwenye gereza."

Binti huyo hatimaye alisema  alikubali kushiriki kwenye shambulio hilo lakini "hakuwahi kuwa na nia ya kufanya hivyo".

Alisema alijeruhiwa baada ya mmoja wa mabinti hao kujilipua na kuishia hospitali ambapo mabomu hayo yaligunduliwa.

Haikuwa rahisi kuthibitisha taarifa ya binti huyo. Waandishi walisema hapakuwa na wakili wowote wakati wa mkutano hao wa waandishi wa habari.

Chanzo: BBC
Imetafsiriwa na Mwandishi wetu

No comments:

Post a Comment