Wednesday, 17 December 2014
BILL COSBY: MASHTAKA YA 1974 KUTOFUNGULIWA
Mashtaka dhidi ya mchekeshaji Bill Cosby hayatofunguliwa juu ya madai kuwa alimdhalilisha kijinsia binti mdogo mwaka 1974, waendesha mashtaka wa Marekani alisema.
Walielezea kuwa kuna kikomo kinachozuia kuchukua hatua za kisheria baada ya muda fulani inapodaiwa kosa hilo kufanyika.
Judy Huth alidai kuwa Bw Cosby alimdhalilisha akiwa na umri wa miaka 15.
Ni miongoni mwa takriban wanawake 15 ambao mapema mwezi Novemba wamedai kuwa Bw Cosby aliwadhalilisha kijinsia.
Mawakili wa mchekeshaji huyo wamekana mengi ya madai hayo huku wengine wakiwapuuza wakisema aidha uongo au madai yamepitwa na wakati.
Wengi wa wanawake hao wanasema mchekeshaji huo aliwalewesha kabla ya kuwadhalilisha.
Bi Huth alidai alilazimishwa na Bw Cosby kumfanyia kitendo cha ngono huko Los Angeles.
Labels:
Habari
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment