Sheria ya kutengeneza watoto kutoka watu watatu – ambapo inasemwa
wawili tu watakuwa wazazi halali- imetangazwa na serikali ya Uingereza.
Mbinu hiyo ya uzalishaji itatumia nasaba kutoka kwa mama,
baba na mwanamke wa kujitolea ili kuzuia maradhi.
Wabunge hivi karibuni watapiga kura ili kuifanya
Uingereza nchi ya kwanza duniani kuhalalisha utaratibu huo au la.
Wapinzani wanasema ni kinyume cha maadili kutengeneza
watoto kutumia asidi nasaba, DNA kutoka watu watatu.
Wanasayansi wa Uingereza walioongoza utafiti huo
wanatarajia kuanza kutumia utaratibu huo mwakani.
No comments:
Post a Comment