Thursday, 25 December 2014

MSIKITI WACHOMWA MOTO SWEDEN



Firemen outside the mosque in Eskilstuna, Sweden, that was set alight - 25 December 2014

Mtu mmoja amechoma moto msikiti katika mji wa Eskilstuna nchini Sweden siku ya Alhamis, na kujeruhi watano, polisi walisema.

Takriban watu 15 hadi 20 walikuwa wakihudhuria swala ya mchana kwenye msikiti huo, ulio ghorofa ya chini, moto huo ulipozuka siku ya Krismasi.

Vyombo vya habari nchini humo vimeonyesha moshi na mvuke ukitoka dirishani kabla ya wazima moto kuutuliza moto huo.

Tukio hilo linatokea huku kukiwa na majadiliano makali Sweden juu ya sera za uhamiaji.

Wafuasi wa mrengo wa kulia wanataka kupunguza watu wanaotaka hifadhi nchini humo kwa 90%, huku vyama vengine vikitaka kudumisha sera za nchi hiyo za kiliberali.

 Msemaji wa polisi Lars Franzell alisema watu watano walipelekwa hospitali kupata matibabu baada ya kujeruhiwa kutokana na kuvuta pumzi wa moshi.

Mpaka sasa hamna aliyekamatwa kutokana na tukio hilo, Bw Franzell alisema.




No comments:

Post a Comment