Korea Kaskazini
inaripotiwa kuamuru mtu yeyote mwenye jina sawa na la kiongozi wake Kim
Jong-un, kubadili mara moja., kulingana na vyombo vya habari vya Korea kusini.
Taarifa kutoka vyombo
vya habari vya Korea Kusini zinasema jina hilo limezuiliwa kupewa kwa watoto wanaozaliwa kuanzia sasa.
Mbali na hilo na wale wanaolitumia, tayari wanalazimika
kubadili vyeti vyao vya kuzaliwa na nyaraka za makazi yao.
Amri hiyo ilitolewa tangu mwaka 2011 lakini ndio kwanza sasa
imetolewa hadharani.
Karibu asilimia ishirini ya familia za Kikorea zina jina
la Kim na Jong-un.
Japo
maelekzo yamenukuliwa kuwa hatua hiyo ni
hiari, waandishi walisema wachache Korea Kaskazini wataacha kutii.
No comments:
Post a Comment