Monday, 15 December 2014
YAYA WA UGANDA AHUKUMIWA
Mfanyakazi wa ndani, Jolly Tumuhirwe, mwenye umri wa miaka 22, amepewa kifungo cha miaka minne gerezani nchini Uganda kwa kumnyanyasa mtoto, katika kesi iliyozua hasira baada ya video kutolewa kwenye mitandao ya kijamii.
Alirekodiwa akiwa anampiga, akimpiga mateke mtoto huyo wa miezi 18.
Siku ya Ijumaa aliiambia mahakama kuwa kilichomchochea kumpiga mtoto huyo ni kufuatia mama wa mtoto huyo kumpiga- jambo ambalo mama wa mtoto huyo amelikataa.
Awali mashtaka ya utesaji yalifutwa baada ya waendesha mashtaka kusema si rahisi kuthibitisha hilo.
'Alinaswa na kamera'
Video ikionyesha utesaji wa mtoto huo ulizua tafrani kubwa iliposambazwa kwenye mitandao ya kijamii.
Baba yake mtoto huyo, Eric Kamanzi, aliweka kamera baada ya kugundua mtoto wake akiwa na majeraha na anaburuza mguu.
Alipofikishwa mahakamani kwa mara ya kwanza mwendesha mashtaka wa serikali Joyce Tushabe aliiambia mahakama kuwa mfanyakazi huyo “anajutia” na kuomba msamaha.
Video hiyo iliyochukuliwa na kamera iliyokuwa imefichwa pembezoni mwa ukumbi, inamwonyesha Tumuhirwe akimpiga mtoto huyo alipokataa kula kisha akamtupa chini kwenye sakafu, huku akimpiga na tochi kabla ya kumkanyaga na kumpiga mateke.
Baada ya kunasa ukatili huyo, baba wa mtoto huyo aliripoti tukio hilo kwa polisi Novemba 13.
Labels:
Habari
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment