Taarifa ikisomwa kwa niaba ya maafisa hao watatu |
Walinzi watatu wa G4S, Uingereza wamekutwa hawana hatia kwa mashtaka ya kuua bila kukusudia wa mtu aliyefariki dunia wakati wa jaribio la kumfurumusha nchini katika uwanja wa ndege wa Heathrow.
Jimmy Mubenga, mwenye umri wa miaka 46, alipata ugonjwa wa moyo baada ya kushikiliwa kwenye ndege, Oktoba 2010.
Terence Hughes, 53, Colin Kaler, 52, na Stuart Tribelnig, 39, walikana kumshughulikia vibaya au kwa kumpuuza wakati wa tukio hilo, kwenye ndege ya Brirish Airways.
Walishutumiwa kwa kuzuia upumuaji wa Mubenga.
Jimmy Mubenga alikuwa akirejeshwa Angola |
Mahakama iliambiwa abiria walimsikia Bw Mubenga akilia "Siwezi kupumua" wakati alipobanwa kwenye kiti – huku tayari akiwa amefungwa pingu kwa nyuma na mkanda pia.
Lakini walinzi hao wamekana kumkandamiza kwenye kiti na kumweka kwenye mkao ulioathiri kupumua kwake.
Pia walisisitiza hawakumsikia akipiga kelele akisema hawezi kupumua
Bw Mubenga alifurumishwa nchini Uingereza kurejeshwa Angola baada ya kutumikia kifungo cha miaka miwili gerezani kwa kudhalilisha na kusababisha majeraha.
Kufuatia uamuzi huo, walinzi hao walisema walifurahishwa sana kufutiwa mashtaka hayo.
No comments:
Post a Comment