Kikombe cha kahawa asubuhi ni kinywaji ambacho wengi wetu huanza nacho.
Kama unahisi bila hiyo huwezi kuanza siku yako vizuri, basi ujue si peke yako.
Miongoni mwa wanataaluma 10,000 walioshiriki kwenye utafiti ulioafanywa na Pressat, asilimia 85 walisema wanakunywa takriban vikombe vitatu vya kahawa kwa siku.
Na takriban asilimia 70 walikiri kuwa ufanyaji wao wa kazi utaathirika bila kupata kikombe cha kahawa.
Inaonekana kunywa kahawa ni jambo la lazima kazini kwa wataalamu wengi. Wanaokunywa zaidi, hadi vikombe vinne kwa siku, ni wenye kazi zenye mikiki zaidi ‘stress’: waandishi wa habari ndio wanaokunywa kahawa, wakifuatiwa na maafisa polisi na walimu.
Utafiti wa hivi karibuni uliofanywa na Chuo Kikuu cha South Carolina kimegundua kuwa mtu asizidishe milligram 200 za caffeine kwa siku, ambazo ni sawa na vikombe vinne vya kahawa.
Kunywa kahawa kwa wingi ili tu kuweza kupambana na tafrani na uchovu wa kazi unaweza kusababisha hatari kwa afya yako, kuanzia kupooza na wasiwasi, na hadi kupata matatizo ya moyo, japo utafiti huo umeonyesha asilimia 62 ya wafanyakazi hawakujua athari za kiafya zinazowakabili.
Kwa wastani utafiti huo umeonyesha kuwa wanaume wanakunywa kahawa zaidi kuliko wanawake lakini zaidi kidogo kwa asilimia 5.
Zifuatazo ni taaluma kumi zinazokunywa sana kahawa, kulingana na utafiti:
- Waandishi wa habari na wafanyakazi wa vyombo vya habari
- Maafisa wa polisi
- Walimu
- Mafundi bomba
- Wauguzi na wafanyakazi wa afya
- Wakurugenzi wa kampuni
- Wauzaji bidhaa kwa njia ya simu
- Watoa huduma za IT
- Wafanyakazi wa maduka ya rejareja
- Madereva
Chanzo: pressat.co.uk
Imetafsiriwa na Mwandishi wetu
No comments:
Post a Comment