Wednesday 10 December 2014

RIPOTI YA UTESAJI ULIOFANYWA NA CIA

Anti-torture protester in Washington (2008)

Umoja wa Mataifa na mashirika ya kutetea haki za binadamu wametoa wito wa kushtakiwa kwa maafisa wa Marekani waliohusika kwa kile ripoti ya bunge la Seneta limeita mahojiano ya “kikatili” ya shirika la kijasusi la nchi hiyo CIA ya washukiwa wa al-Qaeda.

Ujumbe maalum wa Umoja wa Mataifa UN wa haki za binadamu ulisema kumekuwa na “sera ya wazi ulioandaliwa katika viwango vya juu”.

Shirika hilo la CIA limetetea matendo yake katika miaka mingi hasa baada ya mashambulio ya 9/11 yaliyotokea Marekani, likisema lilikuwa likiokoa maisha ya watu.

Rais Barack Obama alisema sasa ni muda wa kusonga mbele.

‘Mashtaka ya jinai'

Mjumbe maalum wa UN kuhusu Haki za Binadamu na Kupambana na Ugaidi Ben Emmerson alisema maafisa waandamizi kutoka utawala wa George W Bush waliopanga na kutekeleza uhalifu lazima washtakiwe, pamoja na CIA na maafisa wa serikali ya Marekani waliohusika na utesaji kama vile ‘waterboarding’.



‘Waterboarding’ ni aina ya utesaji, ambapo maji humwagiwa kwenye kitambaa ambacho mfungwa amefungwa nacho cha uso na sehemu za kupumulia, mtu huhisi kama amezama. Aina hiyo ya utesaji huweza kusababisha maumivu makali sana, huharibu mapafu, ubongo kutokana na kukosa hewa ya oksijeni.

‘Rectal rehydration’ ni kuingiza kiwango kikubwa cha kimiminika kwenye utumbo mnene kwa kutumia dripu. Ni mbinu iliyotumika sana wakati wa Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia. (maana imetolewa motherboard.vice.com)


Mambo makuu kwenye ripoti:       

  • CIA iliwapotosha wanasiasa na umma
  • Takriban watu 26 miongoni mwa 119 waliotiwa kizuizini wanaojulikana wakati wa mpango huo walishikiliwa kimakosa, na wengi waliwekwa kwa miezi mingi kuliko ilivyotakiwa.
  • Mbinu zilizotumika ni pamoja na kunyimwa usingizi mpaka saa 180, mara nyingi kusimama au mikao mengine yenye maumivu makali.
  • Mshukiwa wa al-Qaeda wa Saudi Arabia Abu Zubaydah aliwekwa kwenye jeneza la boxi kwa saa chungu nzima.
  • ‘Waterboarding’ na "rectal rehydration" iliwaumiza sana wafungwa, na kusababisha kama degdege na kutapika.  
  • Kwa habari zaidi bonyeza hapa http://bbc.in/1wcbNME

No comments:

Post a Comment