Bw Kenyatta alichaguliwa mwaka 2013, licha ya kukabiliwa na mashtaka ICC |
Mahakama ya uhalifu wa kivita ICC imempa
kiongozi wa mashtaka katika mahakama hiyo Fatou Bensouda muda wa wiki moja
aondoe mashtaka dhidi ya Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta.
Kama si hivyo ametakiwa awasilishe
taarifa kuelezea ikiwa ana ushahidi wa kutosha kuendeleza kesi hiyo.
Mahakama hiyo imekataa ombi la kiongozi
huyo wa mashtaka kuiahirisha kesi dhidi ya Bwana Kenyatta ili kumpa muda
kutafuta ushahidi zaidi. Bw Kenyatta alikuwa kiongozi wa kwanza wa nchi kufikishwa rasmi mahakamani tangu kushtakiwa mwaka 2012 kwa uhalifu dhidi ya binadamu, jambo analokataa.
Upande wa mashtaka mara kwa mara umeomba muda zaidi kujenga hoja ya kesi hiyo.
Wamesema mashahidi wamekuwa wakihongwa na kutishwa, na serikali ya Kenya imekataa kukabidhi nyaraka muhimu zinazotakiwa.
Bw Kenyatta amekana kuchochea ghasia kufuatia uchaguzi wenye utata mwaka 2007 ili kuzuia ushindi wa kwa wakati ule Rais Mwai Kibaki na kusema kesi ya ICC ni ya kisiasa.
No comments:
Post a Comment