Tuesday, 9 December 2014

'GHADHABU ZA NJUGU' ZACHELEWESHA NDEGE


This picture taken on 3 September  2014 shows Heather Cho (also known as Cho Hyun-Ah, speaking  in Incheon, west of Seoul
Heather Cho ni binti wa mkuu wa kampuni ya Korean Air

Mkurugenzi wa shirika la ndege la Korean Air anachunguzwa kwa  madai kuwa alichelewesha safari ya ndege kutokana na namna alivyopewa njugu.

Heather Cho alitaka mfanyakazi mmoja wa ndege hiyo atolewe kwenye chombo hicho, Ijumaa iliyopita kwa kushindwa kumpa njugu zikiwa kwenye sahani.

Bi Cho, makamu wa rais wa kampuni hiyo, aliilazimisha ndege hiyo irejee ilipokuwepo mjini New York.

Kampuni hiyo ilisema kuangalia viwango vya huduma za ndege ni sehemu ya kazi ya Bi Cho, na aliungwa mkono na rubani. Lakini maafisa wanasema kwa wakati huo alikuwa ni abiria.

Vyombo vya habari nchini humo vimeripoti kuwa alisema mfanyakazi wa ndege hiyo alimpa Bi Cho njugu aina ya macadamia kwenye mfuko, badala ya kuziweka kwenye sahani.

Bi Cho, binti wa mkuu wa kampuni hiyo Cho Yang-ho, kisha akamhoji mkuu wa wafanyakazi kuhusu viwango vya huduma za ndege na kumwaamuru ashuke kwenye ndege.

Korean Air ilisema ndege hiyo ilichelewa kwa dakika 11, na uamuzi wa kumfukuza mfanyakazi huyo mwandamizi ulifanywa kwa makubaliano na rubani.

Mamlaka za usafiri zinachunguza iwapo kitendo cha Bi Cho kimekiuka sheria za usafiri wa anga.

No comments:

Post a Comment