Waendesha mashtaka wa Mahakama ya Kimataifa ya uhalifu wa
kivita ICC mjini the Hague wamefuta mashataka ya uhalifu dhidi ya binadamu
yaliyokuwa yakimkabili Rais Uhuru Kenyatta.
Akishtakiwa kwa kuhusishwa na ghasia za baada ya uchaguzi mwaka 2007/2008 ambapo watu 1,200 walifariki dunia.
Bi Kenyatta, aliyekana mashtaka hayo, alisema alihisi “amefutiwa lawama.”
Ofisi ya waendesha mashtaka ilisema serikali ya Kenya ilikataa kukabidhi ushahidi ulio muhimu katika kesi hiyo.
Bw Kenyatta aliandika kwenye mtandao wa kijamii wa Twitter kuwa alikuwa na “furaha” kufuatia kufutwa kwa mashtaka hayo.
Rais Uhuru Kenyatta na naibu wake William Ruto |
"Nafsi yangu iko safi kabisa," alisema, akiongeza ujumbe mwengine kuwa kesi yake “iliharakizwa kupelekwa huko bila uchunguzi wa kutosha”.
Waziri wa mambo ya nje wa Kenya Amina Mohamed alisema serikali yake itaendelea kushughulikia kesi nyingine mbili kama hizo zifutwe moja ikimhusu Naibu Rais William Ruto.
No comments:
Post a Comment