Thursday, 4 December 2014

RAIS MUGABE AHAMAKI JUU YA 'JARIBIO LA KUMWUUA'



Zimbabwean President Robert Mugabe delivers his speech during the official opening of the Zanu-PF congress in Harare on 4 December 2014

Rais wa Zimbabwe amezungumzia hasira zake juu ya naibu wake walio kwenye mzozo Joyce Mujuru kwa madai ya kula njama ya kumwuua kiongozi huyo na kumtuhumu kuwa mwizi.

Akizungumza katika mkutano wa chama tawala cha Zanu-PF, Robert Mugabe alisema atawashughulikia maafisa wote mafisadi.

Kutokuwepo Bi Mujuru kwenye mkutano huo kunaashiria kuwa “anaogopa” alisema Bw Mugabe.

Siku za hivi karibuni mwanachama wa Zanu-PF aliyefurumushwa Rugare Gumbo aliiambia  BBC kiongozi huyo mwenye umri wa miaka 90 amebadilisha “kabisa” chama hicho kuwa “mali yake binafsi”.

Bw Mugabe alimlenga Bi Mujuru ili ‘kumpembejea’ mke wake Grace, aliyekuwa msemaji wa Zanu-PF aliongeza.

Bi Mujuru, ambaye hivi karibuni alikana madai hayo, alikuwa ana nafasi kubwa ya kumrithi Bw Mugabe, ambaye alikuwa naye sambamba wakati wa kupigania uhuru wa Zimbabwe kutoka kwa wazungu walio wachache.

Hatahivyo, ndoto zake zilianza kuyumba baada ya Bi Mugabe kuingia kwenye siasa mwaka huu, na kumshutumu kwa kupanga jaribio la kumwuua mumewe.

Mkutano huo, unaofanyika mjini Harare, unatarajiwa kumchagua mke huyo wa rais kuwa kiongozi wa umoja wa wanawake wa Zanu-PF.

No comments:

Post a Comment