Sunday 28 September 2014

DENNIS KIMETTO WA KENYA AVUNJA REKODI, BERLIN

Dennis Kimetto

Dennis Kimetto wa Kenya amevunja rekodi ya dunia ya mashindano ya marathon mjini Berlin, akishinda katika kipindi cha saa mbili, dakika mbili na sekunde 57.

Kimetto mwenye umri wa miaka 30 alichomoka kwenye kundi la watu saba wakiwemo wenzake kutoka Kenya Emmanuel Mutai na Geoffrey Kamworor. 

Alifanikiwa kumkimbia Mutai ikiwa zimebaki maili tatu tu na kuwa mtu wa kwanza kushinda marathon chini ya saa mbili na dakika tatu.

"Najisikia vizuri kwasababu nimeshinda katika mchuano mzito sana," alisema Kimetto.

"Nilikuwa najisikia vizuri tangu mwanzo na maili chache za mwisho nilihisi naweza na nitavunja rekodi."

ATI MWANAMKE HUTAFUNA UBANI HIVI?

    

Vimbwanga vya WhatsApp

MALIMA: MTANZANIA ATAKAYEOKOA DUNIA

UMEPATA kusikia jina la Dk. Asanterabi Malima? 
Ansterabi Malima
Jambo moja ambalo wanafunzi waliosoma naye nchini Tanzania hawabishani kuhusu Malima ni ukweli kwamba alikuwa ni mwanafunzi mwenye akili nyingi darasani.

Shafii Dauda ambaye alikuwa mwanafunzi wa kidato cha kwanza katika Shule ya Sekondari Azania jijini Dar es  Salaam, anamkumbuka Asanterabi kama mwanafunzi mwenye akili aliyefanya vizuri sana katika masomo yake ya kumaliza kidato cha nne.

Shafii, ambaye sasa ni miongoni mwa watangazaji na wachambuzi maarufu wa

mchezo wa soka hapa nchini alikuwa kidato cha kwanza wakati Malima alikuwa kidato cha nne.
Akili ile ya Malima imemfikisha nchini Marekani ambako sasa amefanya ugunduzi wa kidude chenye saizi ya pini ndogo (milimita 0.250) kinachoweza kubaini magonjwa ya kuambukiza, kansa na moyo katika hatua ya awali kabisa.

Mtafiti wa Kisayansi

Ugunduzi huu, utakapofika mwisho wake, unaweza kuokoa maisha ya watu wengi duniani. Fikiria tu kwamba unakuwa na kifaa ambacho mojawapo ya magonjwa hayo yakikuanza unaubaini mapema na kwenda kutibiwa.

Mamilioni ya watu wataokolewa maisha yao na kijana huyu wa Kitanzania.

“Siku zote nimekuwa na ndoto za kugundua kitu ambacho kitaweza kuokoa maisha ya watu. Baba yangu alifariki kwa ugonjwa wa moyo ambao ungegundulika mapema kama kungekuwa na kifaa kama hiki.

“Kwa sasa sitaweza kuokoa maisha ya baba yangu lakini ninaweza kuokoa maisha ya wazazi au watoto wa watu wengine kutokana na ugunduzi huu nilioufanya. Nafurahi kwamba ndoto yangu imetimia.

“Kansa, baadhi ya magonjwa ya kuambukizwa na magonjwa ya moyo huwa yanachelewa sana kugundulika. Watu wengi hupoteza maisha, na kwa nchi zilizoendelea hutumia pesa nyingi sana kuwatibu waathirika.

“Kifaa nilichogundua ni kidude cha ukubwa wa pini (0.250mm) kinachoweza kupima na kugundua hayo magonjwa mapema. Ili, yaweze kutibika kirahisi, kuokoa maisha na kupunguza gharama,” anasema

Asanterabi katika mazungumzo yake na Raia Mwema yaliyofanyika kwa njia ya mtandao juzi Jumatatu.

Asanterabi ni mtoto wa aliyepata kuwa waziri wa fedha wa Tanzania, Profesa Kighoma Ali Malima, aliyefariki dunia Agosti 6, 1995 jijini London, Uingereza, katika mojawapo ya vifo vya kushtusha katika historia ya Tanzania.

Kifaa alichokigundia kijana huyu wa Kitanzania kinafahamika kwa jina la Biolom na ugunduzi huu aliufanya akishirikiana na wanafunzi wenzake wawili wa Chuo Kikuu cha Northeastern kilichopo Boston; Cihan Yilmaz na Jaydev Upponi.

Pamoja na udogo wake, kipini hicho kina jumla ya maeneo manne –yote yenye kazi maalumu, na ubunifu huo tayari umetambuliwa na Serikali ya Marekani.

Katika mazungumzo yake na vyombo vya habari vya Marekani, Asanterabi alipata kusema kwamba vifaa vingi vya kisasa hubaini magonjwa; kwa mfano kansa, katika wakati ambapo ni vigumu mtu kupata tiba na kupona.

“Kazi yetu hii itakapokamilika, tutaweza kubaini magonjwa haraka zaidi na mapema zaidi na hivyo watu watapata tiba mapema na kuokoa maisha.

“Nchini kwangu (Tanzania), akinamama wengi hufariki dunia kwa sababu ya kuugua ugonjwa wa kansa ya kizazi, kifaa hiki kitaweza kusaidia watu wengi kupona kutoka katika matatizo yao,” alisema.

Kidude hicho ni kidogo sana kwa umbo na namuuliza kama wameamua iwapo mtu anaweza kukinunua na kubaki nacho nyumbani akijitazama mwenyewe au ni lazima aende hospitali.

“Dhamira yetu hapo ni kipimo kitumike mtu akienda hospitali au kliniki (for annual check-up). Lakini japokuwa kinafanya kazi, kupata ruhusa kwa kukiingiza kama pini ni vigumu. Tunafanya vipimo (test) kwa kupima damu iliyotoka kwa mgonjwa,” anasema.

 Elimu yake

NYOTA WA FILAMU GEORGE CLOONEY AFUNGA NDOA



George Clooney and his fiancee Amal Alamuddin arrive in Venice, 26 September

Nyota muigizaji wa Hollywood George Clooney amemwoa mwanasheria wa kutetea haki za binadamu  Amal Alamuddin huko Venice, miongoni mwa matukio yaliyokuwa yakisubiriwa kwa hamu zote.

Wenzake ambao ni maarufu pia kwenye tasnia ya uigizaji na uimbaji katika mji wa Italia walimiminika kushuhudia muungano huo wa kapera maarufu katika uwanda wa filamu, mwenye umri wa miaka 53, na Bi Alamuddin, mwenye umri wa miaka 36.

Shughuli hiyo ilisherehekewa katika hoteli iliyoelekea kwenye mfereji mkubwa wa Venice.

Wakala wa Clooney walitoa taarifa hiyo kwa waandishi wa habari.

Kulingana na shirika la habari la AP, hiyo ndio itakuwa taarifa pekee itakayotolewa kuhusu harusi hiyo.




Saturday 27 September 2014

HUKUMU YA HOSNI MUBARAK KUTOLEWA KARIBUNI

Former Egyptian president Hosni Mubarak is wheeled out of an ambulance outside the Maadi military hospital in Cairo (27 September 2014)
Mubarak alisafirishwa kwa helikopta ya jeshi kufikishwa mahakamani siku ya Jumamosi

Mahakama ya Misri inatarajia kutoa uamuzi kwenye kesi inayomkabili aliyekuwa Rais wa Misri  Hosni Mubarak kwa makosa ya rushwa na kuua waandamanaji wakati wa ghasia za mwaka 2011.

Mubarak, mwenye umri wa miaka 86, anashtakiwa pamoja na watoto wake wa kiume na aliyekuwa waziri.

Alikutwa na hatia na kuhukumiwa kifungo cha maisha mwaka 2012, lakini hukumu hiyo baadae ilibadilishwa.

Mubarak aliiongoza Misri kwa takriban miaka 30 kabla ya ghasia kuibuka na kuondolewa.

Aliachia madaraka baada ya wiki kadhaa za vurugu zilizosababisha vifo vya mamia ya waandamanaji nchini humo.

Kesi hiyo mpya ilianza Aprili 2013, na imeahirishwa mara chungu nzima.

Wachambuzi wanasema Mubarak huenda akaachiwa huru, baada ya mashahidi wengi kubadilisha ushahidi wao na ukiegemea upande wake.

Mubarak tayari anatumikia miaka mitatu gerezani kwa ubadhirifu wa mali ya umma.

Alikutwa na hatia mwaka 2012 kwa mashtaka yanayohusiana na mauaji ya waandamanaji pamoja na aliyekuwa waziri wa mambo ya ndani Habi al-Adly, na kuhukumiwa kifungo cha maisha.

Watoto wake wa kiume Alaa na Gamal nao kwa sasa wanatumikia kifungo cha miaka minne jela kwa ubadhirifu wa mali za serikali.

Pamoja na baba yao walitozwa faini $3m na kuamriwa kurejesha $17.6m waliotuhumiwa kuiba.


CHELSEA CLINTON AJIFUNGUA MTOTO WA KIKE

Chelsea Clinton (September 2014)
Mtoto wa Chelsea ni mjukuu wa kwanza wa Bill na Hillary Clinton

Chelsea Clinton, binti wa aliyekuwa Rais wa Marekani Bill Clinton na aliyekuwa waziri wa mambo ya nje wa nchi hiyo Hillary Clinton, amejifungua mtoto wa kike.

"Mimi na Marc tuna mapenzi, furaha na tunatoa shukran wakati tukisherehekea kuzaliwa kwa binti yetu, Charlote Clinton Mezvinsky, " Bi Clinton aliandika kwenye mtandao wa kijamii wa twitter.

Bi Clinton, mwenye umri wa miaka 34, aliolewa na Marc Mezvinsky mwaka 2010, na kutangaza kuwa mjamzito Aprili 2014.

Binti huyo anazaliwa huku Bi Hillary Clinton akiwa na nia ya kugombea urais mwaka 2016.

Anaonekana kuwa mgombea mkuu kupitia chama cha Democrat na mrithi wa Rais Barack Obama, na alisema atachukua uamuzi wa kugombea au la mwanzoni wa mwaka 2015.

Bill Clinton alikuwa rais wa 42 Marekani , kuanzia Januari 1993 hadi Januari 2001.

Chelsea Clinton, alisomea vyuo vikuu vya Stanford, Columbia na Oxford, anasimamia Wakfu wa Clinton akishirikiana na wazazi wake.

Bi Clinton aliacha kazi iliyokuwa ikimlipa $600,000 kwa mwaka kama mwandishi maalum wa habari wa NBC mwezi Agosti ili ashughulike na ujauzito wake.


WACHEZA KRIKETI WAWEKA REKODI MLIMA KILIMANJARO

http://taarifa.co.tz/wp-content/uploads/2014/09/klmm.jpg
Kupumua na kukimbia kuna uziyo kwenye sehemu hiyo ya juu

Kundi la wacheza kriketi wa kimataifa wameweka rekodi mpya ya dunia kwa kucheza mechi kubwa kwenye kilele cha Kilimanjaro, mlima mrefu zaidi Afrika, uliopo nchini Tanzania.

Timu hizo zinamhusisha mrusha mpira wa zamani wa Afrika Kusini Makhaya Ntini na mrusha mpira wa zamani wa England, Ashley Giles.

Mechi hiyo ilichezwa kwenye urefu wa mita 5,730 (futi 18,799) kwenye eneo lilinyooka chini kidogo ya kilele.
Kulikuwa na hali ya baridi na kuganda kwa barafu kwenye eneo hilo.
Kulikuwa na hali ya baridi na kuganda kwa barafu kwenye eneo hilo
        
Hii kweli maajabu! Tunacheza kriketi kwenye kilele cha Afrika, Giles alituma ujumbe kwenye Twitter.

Rekodi ya hivi karibuni ya mechi kubwa ni ile mita 5,165, iliyochezwa kwenye milima ya Himalaya, kwenye kambi ya mlima Everest nchini Nepal mwaka 2009.

Chanzo: taarifa.co.tz

Friday 26 September 2014

AMA KWELI UZEE MWISHO CHALINZE

   

Vimbwanga vya WhatsApp

WENYE MATATIZO YA AKILI KUONGEZEKA, UGANDA



Wataalamu wametoa wito wa kushirikiana zaidi kwa huduma za watu wenye matatizo ya akili na huduma na tiba kwa walioathirika na Ukimwi na huduma ya afya kwa jumla.

Wito huo umetolewa baada ya idadi ya watu wenye matatizo ya akili kuongezeka nchini Uganda hasa watu wanaoishi na Ukimwi.

Dk Sheila Ndyanabangi, afisa mkuu wa tiba wa wenye matatizo ya akili katika wizara ya afya, alisema idadi ya watu wenye matatizo ya akili kuripotiwa imeongezeka kwa 17,000 kati ya mwaka 2009 hadi 2012.

Alisema idadi hiyo inatokana na migogoro ya hivi karibuni na kupanuka kwa miji iliyowalazimu watu wengi kujihusisha na kamari na kukopa mara kwa mara, pamoja na matumizi ya pombe na dawa za kulevya.

Takriban 56% ya Waganda wanaoishi na virusi vya HIV wana msongo wa mawazo, na dalili kama kulala kwa tabu, kutokuwa na hamu ya kula, na kusikia uchovu mara zote.

Dalili nyingine ni huzuni, na kuzongwa na mawazo yaliyojaa matatizo. Japo si jambo linalotokea sana, baadhi ya watu huzidiwa na msongo wa mawazo mpaka hutaka kujiua.


Chanzo: New vision, Uganda 

Thursday 25 September 2014

ASAMOAH GYAN AKANA KUMTOA RAFIKI YAKE 'KAFARA'




Kapteni wa Ghana Asamoah Gyan alisema madai kuwa alimwuua rafiki yake ambaye ni msanii wa miondoko ya hip-hop Castro kama sehemu ya kafara ni “ upuuzi mtupu”.

Msanii Castro, ambaye jina lake halisi ni Theophilus Tagoe, alitoweka , pamoja na rafiki yake Janet Bandu,mwezi Julai.

Walitoweka walipoenda likizo na familia ya mshambuliaji huyo wa zamani wa Sunderland , Gyan katika mji wa Ada kwenye pwani ya Ghana.

Madai yaliyotolewa na vyombo vya habari vya Ghana vinasema kutoweka huko kunaonyesha mazingira ya utata.

Castro na Bandu mara ya mwisho walionekana wakielekea kwenye pwani hiyo kwenye motokari ya majini ‘jet ski’ na baadae kutangazwa kuwa walizama.

Castro

Hakuna miili yoyote iliyoopolewa mpaka sasa na uvumi uliendelea kusambazwa mwezi huu baada ya kaka yake, Baffour Gyan, akidaiwa kuwa sehemu ya genge lililomshambulia mwandishi wa habari aliyemhoji mchezaji huyo kuhusu uvumi huo.

Kwa sasa hata hivyo,  Baffour Gyan amefutiwa makosa yake.

Hisia hizo zilisababisha Gyan mwenye umri wa miaka 28 aliyejiunga na Al-Ain ya UAE mwaka 2011, kufanya mkutano na waandishi wa habari.

Wakili wake Kissi Agyabeng alisema familia yake imepata "mshtuko" na wamebaki kimya mpaka sasa kwa kuwa hawakutaka kuingilia uchunguzi wa polisi.

"MBU WAZURI" KUPAMBANA NA DENGE - BRAZIL

Watafiti wa Brazil mjini Rio de Janeiro wamewatawanya maelfu ya mbu walio na bakteria anayefubaza homa ya dengu.

Matumaini ni kuwa watazaliana, na kuongezeka kwa wingi, hivyo kupunguza watu wanaopata ugonjwa huo.

Mchakato huo ni sehemu ya mradi unaofanyika pia Australia, Vietnam na Indonesia.

Bakteria huyo, Wolbachia, hawezi kuingiziwa kwa binadamu

Mradi huo ulianza mwaka 2012 alisema Luciano Moreira wa taasisi ya utafiti ya Brazil iitwayo Fiocruz, ambaye ndiye anasimamia utafiti huo.

Alisema maelfu ya mbu hao wataachiwa wazunguke wanapotaka kila mwezi kwa muda wa miezi minne, mwanzo wakianzia Tubiacanga, kaskazini mwa Rio.

Bakteria "Wazuri'

Bakteria Wolbachia anapatikana kwenye wadudu kwa 60%. Hufanya kazi kama kinga kwa mbu anayehifadhi denge, Aedes aegypti, akizuia virusi vya dengu kuzaliana mwilini.

Wolbachia pia ana athari yake kwenye uzalishaji. Ikatokea mbu dume aliye na virusi hivyo akarutubisha mayai ya jike bila ya bakteria hao, mayai hayo hayaingii kwenye hatua ya lava.

Iwapo wote jike na dume wakiwa na virusi hivyo au kama jike tu ndio ana bakteria, vizazi vyote vya siku za usoni vya mbu hao watakuwa na Wolbachia.

Kwa matokeo hayo, mbu wa Aedes ambao wana Wolbachia wanakuwa wengi bila hata watafiti kuendelea kuwasambaza wadudu walioathirika kila mara . Maradhi ya dengu yaliibuka upya Brazil mwaka 1981 baada ya kutoweka kabisa kwa zaidi ya miaka 20.

Baada ya miaka 30 iliyofuata, watu milioni saba waliripotiwa kuathirika.

Brazil inaongoza duniani kwa idadi ya watu walioathirika na denge, huku wakiwepo watu milioni 3.2 walioathirika na 800 kufariki kutokana na ugonjwa huo baina ya mwaka 2009 - 2014.

Chanzo: BBC
Imetafsiriwa na Mwandishi wetu


MENDE HAFUGWI TU, HULIWA HASA

 

Vimbwanga vya WhatsApp     

Wednesday 24 September 2014

BOKO HARAM WAJISALIMISHA, MKUU 'ADAIWA' KUUAWA

Boko Haram video with alleged leader whose death is disputed 24 August 2014

Jeshi la Nigeria limesema zaidi ya wapiganaji 260 wa Boko Haram wamejisalimisha kaskazini-mashariki mwa nchi hiyo.

Msemaji pia alisema jeshi limemwuua aliyekuwa kiongozi wa kundi hilo, Abubakar Shekau.

Mohammed Bashir inasemekana alitokea kwenye video ikionyesha kundi  hilo lakini anahisiwa kuwa si Shekau halisi.

Boko Haram limepoteza wapiganaji wengi katika wiki za hivi karibuni wakati jeshi la Nigeria likipambana nao karibu na makazi yao makuu Maiduguri, kaskazini -mashariki mwa nchi hiyo.

Jeshi hilo lilisema wafuasi 135 wa Boko Haram walijisalimisha pamoja na silaha zao Biu, jimbo la Borno, siku ya Jumanne - na wengine 133 huko kaskazini-mashariki mwa Nigeria ambapo kwa sasa wanahojiwa.

Mwandishi wa BBC Will Ross aliyopo Lagos alisema hatua kama hii haijawahi kutokea tangu vita vya kupambana na Boko Haram kuanza.

Licha ya kwamba ni vigumu kuthibitisha, jeshi linaona tukio hili kuwa jambo lenye umuhimu sana.

KIUMBE CHA AJABU KUIBUKA PEMBA





Katika hali isiyo ya kawaida huko maeneo ya bahari ya Shamiani (kwa Gombe) jimbo la kiwani mkoa wa kusini Pemba kumeibuka kiumbe kikubwa cha ajabu kutoka baharini ambacho kimepwewa.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa baadhi ya wakaazi wa maeneo ya jirani na eneo hilo ambao wamefurika kwa wingi kwenda kuona kiumbe hicho wamesema kuwa ni mara ya kwanza kuona kiumbe cha namna hicho kikiwa kimepwewa ndani ya bahari.

Baadhi yao wameeleza kuwa huenda pengine kiumbe hicho cha ajabu chenye urefu takribani mita 40 na upana zaidi ya mita 25 kikawa ni samaki aina ya nyangumi au chongowe.

Katika hali ya kushangaza ndani ya fukwe hizo za bahari ya kwa Gombe watu zaidi ya 200 kutoka maeneo jirani ya Likoni,mwambe na ngambu shamiani wamejitokeza kuona kiumbe hicho cha ajabu ambacho tayari kimekufa.

Aidha makundi ya wananchi wanaendelea kukata minofu ya aina hiyo ya kiumbe huku wengine wakijaza madumu yao mafuta yanayotiririka kutoka kwa kiumbe hicho.

Kwa upande wake mtalamu wa viumbe vya bahari Zanzibar kwa masharti ya kutotajwa jina amesema msimu huu viumbe vya bahari aina ya nyangumi hupita katika ukanda wa bahari ya hindi.

“Inaonekana baadhi ya watu huwapiga viumbe vya bahari vya aina hii ndio maana hufariki dunia,hali hii inaitia nchi yetu jina baya kimataifa tunaonekana tunawaua kwa makusudi’’aliongezea mtaalamu huyo.

Alieleza kuwa kitengo chao kimeshatoa elimu sana ili wananchi waache tabia hii ya kuwaangamiza viumbe hawa kwani dunia haikubali kwa sasa kwa vile ni viumbe adimu na muhimu. 

Aidha alieleza alishauri wananchi wakiona kiumbe kama hicho kikiwa hai basi watoe taarifa kwa wahusika ili aweze kurudishwa baharini.

Hali hii ya kuonekana kiumbe cha ajabu ni mara ya kwanza kwa maeneo haya ambapo kumeibua mshangao.

Chanzo: WhatsApp

ABU QATADA AFUTIWA MASHTAKA YA UGAIDI



Abu Qatada stands behind bars
Abu Qatada alishtakiwa kwa jaribio la kuwashambulia Waisraeli, Wamarekani na wengine wa nchi za magharibi

Mhubiri wa Kiislamu mwenye msimamo mkali Abu Qatada amekutwa hana hatia ya makosa ya kigaidi na mahakama ya Jordan.

Jopo la majaji wa kiraia wa mahakama ya Amman wamemfutia mashtaka ya kuhusika katika jaribio la kufanya shambulio lililokusudiwa katika sherehe za millennia mwaka 2000.

Uamuzi huo unatolewa baada ya kufutiwa mashtaka mwezi Juni ya jaribio la kufanya shambulio kwa kutumia mabomu nchini Jordan mwaka 1998.

Abu Qatada alihamishwa kutoka Uingereza mwaka 2013.

Uamuzi huo unafuatia msuguano wa kisheria wa muda mrefu baina ya mawaziri nchini Uingereza kulazimisha mhubiri huyo kushtakiwa kwao Jordan.

Japo atakuwa huru siku za hivi karibuni, hatorejea London.

Mhubiri huyo, ambaye jina lake halisi ni Omar Othman, alipewa hifadhi Uingereza mwaka 1994, lakini shirika la usalama MI5 lilizidi kumwona tishio kwa usalama wa taifa.