Wednesday, 24 September 2014
BOKO HARAM WAJISALIMISHA, MKUU 'ADAIWA' KUUAWA
Jeshi la Nigeria limesema zaidi ya wapiganaji 260 wa Boko Haram wamejisalimisha kaskazini-mashariki mwa nchi hiyo.
Msemaji pia alisema jeshi limemwuua aliyekuwa kiongozi wa kundi hilo, Abubakar Shekau.
Mohammed Bashir inasemekana alitokea kwenye video ikionyesha kundi hilo lakini anahisiwa kuwa si Shekau halisi.
Boko Haram limepoteza wapiganaji wengi katika wiki za hivi karibuni wakati jeshi la Nigeria likipambana nao karibu na makazi yao makuu Maiduguri, kaskazini -mashariki mwa nchi hiyo.
Jeshi hilo lilisema wafuasi 135 wa Boko Haram walijisalimisha pamoja na silaha zao Biu, jimbo la Borno, siku ya Jumanne - na wengine 133 huko kaskazini-mashariki mwa Nigeria ambapo kwa sasa wanahojiwa.
Mwandishi wa BBC Will Ross aliyopo Lagos alisema hatua kama hii haijawahi kutokea tangu vita vya kupambana na Boko Haram kuanza.
Licha ya kwamba ni vigumu kuthibitisha, jeshi linaona tukio hili kuwa jambo lenye umuhimu sana.
Labels:
Habari
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment