Sunday, 14 September 2014

'WAARABU WATOA MSAADA' WA KUPAMBANA NA IS



US Secretary of State John Kerry boards his plane at Cairo International Airport on 13 September 2014 as he leaves the Egyptian capital.
John Kerry amekuwa akisafiri Mashariki ya Kati kutaka kuungwa mkono kupamabana na IS

Nchi kadhaa za Kiarabu zimejitolea kufanya mashambulio ya anga dhidi ya wapiganaji wa Islamic State (IS) nchini Iraq, maafisa wa Marekani wamesema.

Lakini hamna hatua yoyote itakayochukuliwa mpaka iidhinishwe na serikali ya Iraq, walisema.

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani John Kerry amesmea “ana imani kubwa” na ahadi zilizotolewa za misaada ya kijeshi za kupambana na kundi hilo.

Alizungumza mjini Paris baada ya ziara ya kasi Mashariki ya Kati kujaribu kushawishi nchi kadhaa kuwaunga mkono ili kupambana na IS.

Ufaransa ina mpango wa kufanya mkutano wa kimataifa kuzungumzia usalama wa Iraq na namna ya kupambana na IS siku ya Jumatatu.

Siku ya Jumamosi, kundi hilo lilitoa video ikionyesha kumkata kichwa mateka wa Uingereza David Haines. Kundi hilo limetishia kumwuua Mwingereza wa pili, Alan Henning, ambaye pia alitokea kwenye video hiyo.

Chanzo: BBC
Imetafsiriwa na Mwandishi wetu

No comments:

Post a Comment