Wednesday 24 September 2014

ABU QATADA AFUTIWA MASHTAKA YA UGAIDI



Abu Qatada stands behind bars
Abu Qatada alishtakiwa kwa jaribio la kuwashambulia Waisraeli, Wamarekani na wengine wa nchi za magharibi

Mhubiri wa Kiislamu mwenye msimamo mkali Abu Qatada amekutwa hana hatia ya makosa ya kigaidi na mahakama ya Jordan.

Jopo la majaji wa kiraia wa mahakama ya Amman wamemfutia mashtaka ya kuhusika katika jaribio la kufanya shambulio lililokusudiwa katika sherehe za millennia mwaka 2000.

Uamuzi huo unatolewa baada ya kufutiwa mashtaka mwezi Juni ya jaribio la kufanya shambulio kwa kutumia mabomu nchini Jordan mwaka 1998.

Abu Qatada alihamishwa kutoka Uingereza mwaka 2013.

Uamuzi huo unafuatia msuguano wa kisheria wa muda mrefu baina ya mawaziri nchini Uingereza kulazimisha mhubiri huyo kushtakiwa kwao Jordan.

Japo atakuwa huru siku za hivi karibuni, hatorejea London.

Mhubiri huyo, ambaye jina lake halisi ni Omar Othman, alipewa hifadhi Uingereza mwaka 1994, lakini shirika la usalama MI5 lilizidi kumwona tishio kwa usalama wa taifa.


No comments:

Post a Comment