Kupatikana kwa wengine walionusurika kulichochea harakati za msako kuendelea |
Takriban raia 67 wa Afrika kusini walifariki dunia baada ya kanisa linalomilikiwa na mhubiri TB Joshua lilipoporomoka mjini Lagos wiki iliyopita, Rais wa Afrika kusini Jacob Zuma amesema.
Haijulikani ni idadi ya watu wangapi wamekufa kwa jumla, lakini idadi ya mwanzo iliyotolewa ni watu 60.
Ni tukio baya kabisa kuwahi kutokea lililohusisha raia wa Afrika kusini walio nje ya nchi "katika historia yetu", alisema Bw Zuma.
Bw Joshua, mhubiri maarufu sana kutoka Nigeria, anajulikana Afrika nzima.
Bw Joshua alisema ndege ndogo ilikuwa ikizunguka juu ya jengo hilo kabla ya kuporomoka siku ya Ijumaa mchana, na kusema lilikuwa jaribio la kumwuua.
Hatahivyo, siku ya Jumanne, afisa wa uokoaji alisema inaonyesha sababu ya kuporomoka kwa jengo hilo ni kuongeza ujenzi kwa juu kabla ya kuimarisha msingi.
Takriban watu 130, wakiwemo raia wengi wa kigeni, walitolewa kwenye kifusi.
Bw Joshua, ambaye pia anajulikana kama mtume, huwahubiriwa watu wengi sana katika makanisa makubwa wilaya ya Ikotuna mjini Lagos.
No comments:
Post a Comment