Sunday, 21 September 2014

NYUMBA MPYA YA BIG BROTHER YAPATIKANA

 

Nyumba mpya ya Big Brother imepatikana mjini Johannesburg, Afrika kusini, kufutaia moto mkubwa uliozuka na kuteketeza kabisa nyumba ya awali tarehe 2 Septemba.

M-Net na waandaaji wa Big Brother Endemol wamethibitisha hilo, sehemu ya tisa katika kipindi hicho cha televisheni ambacho hurushwa moja kwa moja kitaanza kuonyeshwa tarehe 5 Oktoba, ambacho kitaitwa Big Brother Hotshots.

Kipindi hicho kilitakiwa kianze tarehe 7 Septemba, chenye washindani kutoka nchi 12 za bara la Afrika tayari wakiwa katika hoteli mbalimbali mjini Johannesburg wakiwa tayari kuingia kwenye nyumba hiyo.

Lakini katika tukio la ajabu, taarifa ziliibuka ghafla Afrika kuwa nyumba hiyo imewaka moto, na kipindi hicho kusogezwa mbele.

Msako wa kutafuta nyumba nyingine ukaanza, huku wanaoandaa kipindi hicho wakianza kufikiria mbadala wa kurusha kipindi hicho nchi nyingine ya Afrika, kufuatia wito kutoka kwa wapenzi wa kipindi hicho kiwape nafasi nchi nyingine kuandaa.

Awali, washiriki kutoka nchi 14 za Afrika walitakiwa kuwepo, lakini kutokana na matatizo kwenye hati za kusafiria kutoka washiriki wa Rwanda na Sierra Leone, nchi hizo mbili zikafutwa na kubaki nchi 12.

Iwapo kuchelewa kuanzakwa  kipindi hicho kutawapa nafasi nchi hizo mbili haijajulikana bado.

Mshindi wa Big Brother anatarajiwa kuzawadiwa $300,000

Chanzo: New Vision, Uganda
Imetafsiriwa na Mwandishi wetu

No comments:

Post a Comment