Monday, 15 September 2014
POLISI YAKAMATA 'MABOMU YA AL-SHABAB' UGANDA
Polisi nchini Uganda wamesema wamekamata kiwango kikubwa cha mabomu wakati wa uvamizi eneo la washukiwa wa al-Shabab.
Mamlaka zinasema chumba cha magaidi hao kilikuwa kinapanga kufanya mashambulio kwenye mji mkuu Kampala.
Watu 19 wamekamatwa na kuhojiwa juu ya nia zao, msemaji wa polisi alisema.
Uganda imekuwa katika tahadhari ya hali ya juu tangu kiongozi wa al-Shabab, Ahmed Abdi Godane, alipouawa katika shambulio la anga nchini Somalia mapema mwezi huu.
Wiki iliyopita, ubalozi wa Marekani mjini Kampala ulionya kuwepo uwezekano wa mashambulio ya kulipiza kisasi dhidi ya Wamarekani nchini humo kutokana na shambulio la anga walilofanya Septemba 2.
Siku ya Jumapili, Marekani ilifuta onyo hilo baada ya kusema inaamini “tishio la moja kwa moja la kushambuliwa na al-Shabab limekabiliwa vilivyo”.
Chanzo: BBC
Imetafsiriwa na Mwandishi wetu
Labels:
Habari
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment