Huyu ni mshukiwa wa kuwa mpiganaji na kumwagiwa plastiki iliyoyeyushwa mgongoni mwaka 2013 |
Mateso yamekuwa mazoea kwa polisi nchini Nigeria kiasi ambacho baadhi ya vituo vina afisa asiye rasmi wa kutoa mateso, shirika la kimataifa la kutetea haki za binadamu, Amnesty limesema.
Wote wapiganaji na polisi wanatumia mbinu mbalimbali za kutesa ikiwemo kupiga, kumng'oa mtu kucha na meno na unyanyasaji mwengine wa kijinsia, limesema.
Mwanamke mmoja aliyeshutumiwa mjini Lagos alisema kanyanyaswa kijinsia, na kupuliziwa mabomu ya kutoa machozi kwenye viungo vyake vya uzazi.
Serikali ya Nigeria bado haijasema lolote kuhusu ripoti hiyo.
Kuna mateso ya kumwagiwa maji ya moto na baridi ukiwa utupu |
Mauaji ya holela
Kupewa mateso hutumika sana kaskazini-mashariki katika vita dhidi ya wapiganaji wa Boko Haram, Amnesty ilisema.
Shirika hilo lenye makao makuu yake Uingereza limesema kati ya watu 5,000 na 10,000 wamekamatwa tangu mwaka 2009, na mauaji katika vizuizi vilivyojazana watu ni jambo la kawaida.
Kijana huyu, kwenye picha ya hapo juu, ni miongoni mwa watu 50 waliokamatwa na jeshi katika jimbo la Yobe mwaka jana kwa kushukiwa kuwa sehemu ya Boko Haram.
Wakati huo alikuwa na umri wa miaka 15 na kuwekwa kizuzizini kwa wiki tatu huko Damturu, alisema alipigwa mfululizo na virungu, tako la bunduki na mapanga.
Chanzo: BBC
Imetafsiriwa na Mwandishi wetu
No comments:
Post a Comment