Friday, 26 September 2014

WENYE MATATIZO YA AKILI KUONGEZEKA, UGANDA



Wataalamu wametoa wito wa kushirikiana zaidi kwa huduma za watu wenye matatizo ya akili na huduma na tiba kwa walioathirika na Ukimwi na huduma ya afya kwa jumla.

Wito huo umetolewa baada ya idadi ya watu wenye matatizo ya akili kuongezeka nchini Uganda hasa watu wanaoishi na Ukimwi.

Dk Sheila Ndyanabangi, afisa mkuu wa tiba wa wenye matatizo ya akili katika wizara ya afya, alisema idadi ya watu wenye matatizo ya akili kuripotiwa imeongezeka kwa 17,000 kati ya mwaka 2009 hadi 2012.

Alisema idadi hiyo inatokana na migogoro ya hivi karibuni na kupanuka kwa miji iliyowalazimu watu wengi kujihusisha na kamari na kukopa mara kwa mara, pamoja na matumizi ya pombe na dawa za kulevya.

Takriban 56% ya Waganda wanaoishi na virusi vya HIV wana msongo wa mawazo, na dalili kama kulala kwa tabu, kutokuwa na hamu ya kula, na kusikia uchovu mara zote.

Dalili nyingine ni huzuni, na kuzongwa na mawazo yaliyojaa matatizo. Japo si jambo linalotokea sana, baadhi ya watu huzidiwa na msongo wa mawazo mpaka hutaka kujiua.


Chanzo: New vision, Uganda 

No comments:

Post a Comment