Wapiga kura hawa wawili kusini mwa Edinburgh ni miongoni mwa watu wa mwanzo kuamua khatma ya Uskochi |
Raia wa Uskochi wameanza kupiga kura iwapo nchi hiyo ibaki kwenye muungano au liwe taifa huru.
Wapiga kura watajibu "Ndio" au "Hapana" kwa swali la: "Je Uskochi liwe taifa huru?"
Nchi hiyo ikiwa na watu 4,285,323 - 97% wamejiandikisha kupiga kura- na inatarajiwa idadi kubwa ya watu watajitokeza.
Kura zitapigwa katika vituo 2,608 nchini kote hadi saa nne usiku, siku ya Alhamis,
Matokeo yanatarajiwa kutolewa Ijumaa asubuhi na mapema.
Kura hizo zitahesabiwa katika ofisi 32 za manispaa nchini humo
No comments:
Post a Comment