Aliyekuwa meneja wa Man United, David Moyes |
Manchester
United imetangaza kuporomoka kwa faida ya kila mwaka wa fedha katika mwaka
ambao David Moyes alikuwa meneja.
Klabu
hiyo ya Ligi Kuu ya England imesema kipato halisi kimeporomoka kwa asilimia 84
na kufikia takriban dola milioni 45.
Klabu hiyo imesema inatarajia mapato yake
ya mwaka 2015 kushuka kutokana na klabu hiyo kushindwa kufuzu kucheza Klabu
Bingwa Ulaya kwa mara ya kwanza tangu msimu wa mwaka 1994-95.
Klabu hiyo
imesema Moyes na wasaidizi wake walilipwa zaidi ya dola milioni 8 kama fidia
kufuatia kufukuzwa kazi mwezi Aprili, chini ya mwaka mmoja tangu apewe kazi
hiyo.
Chanzo: FB - Salim Kikeke
No comments:
Post a Comment