Thursday, 18 September 2014
NICK CANNON AVAA VIATU VYA $2 MILIONI
Mariah Carey huenda ndiye akawa anapenda almasi, lakini ni Nick Cannon aliyevaa vito vyenye thamani ya dola za kimarekani milioni 2.
Aaah, kabisa, Bw Cannon, mwenye umri wa miaka 33, amevaa viatu vyenye almasi tupu katika kipindi cha mwisho cha America's Got Talent.
Viatu hivyo vyenye gharama kubwa mno vimetengenezwa na Jason Arasheben, muasisi wa biashara ya vito ya Jason of Berverly Hills.
"Si aghlabu kupata ombi la kutaka kutengenezewa viatu vya gharama kuliko vyote duniani. Nick aliponifuata mwaka jana, alisema anataka kuweka historia na hivyo kufanya jambo zito," alisema.
"Alitaka kuweka kiwango cha kipekee kwenye almasi. 'Tunawezaje kutengeneza viatu vyenye gharama kubwa kupita kiasi dunaini na kumaliza kipindi hichi maalum kwa kishindo?"
Lakini viatu hivi vinavyon'gara, ambavyo inaripotiwa Kitabu cha Kuvunja Rekodi cha Dunia cha Guinness kinatahmini iwapo ni viatu vya gharama duniani, si vyepesi.
Bahati nzuri Nick ana misuli mizito na hata mbunifu alijitahidi kufanya wepesi asitaabike sana.
Chanzo: eonline.com
Imetafsiriwa na Mwandishi wetu
Labels:
Burudani
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment