Katika baadhi ya nchi kuna madakatari wachache sana wa kutibu maradhi ya Ebola |
Madaktari, wauguzi na wataalamu wa kudhibiti maambukizi wataenda Sierra Leone mwezi Oktoba na kukaa kwa muda wa miezi sita.
Tangazo hilo limetolewa huku shirika la Afya Duniani WHO likisema wagonjwa wapya wanaongezeka haraka, hivyo kushindwa kuhimili idadi kubwa ya walioathirika.
Zaidi ya watu 2,400 wamefariki dunia kutokana na virusi hivyo miezi ya karibuni na takriban watu 4,700 wameambukizwa.
Idadi kubwa ya waliokufa ni kutoka Liberia, Sierra Leone na Guinea.
Maafisa wa WHO wamesema idadi ya watu waliofariki dunia bila shaka ni kubwa zaidi kuliko inavyokadiriwa sasa.
Nchini Liberia wataalamu walisema hakuna hata kitanda kimoja kilichobaki cha kuwalaza wagonjwa wa Ebola.
No comments:
Post a Comment