Saturday, 20 September 2014

MAZISHI KWA TEKNOLOJIA

 kifo pix

Kifo ni 'biashara' kubwa
Ikiwa zaidi ya watu nusu milioni hufariki dunia Uingereza kila mwaka, biashara ya mazishi inatengeneza takriban dola bilioni mbili katika mapato ya kila mwaka, kulingana na kampuni ya utafiti ya masoko Ibis World.

Takriban makampuni 1,500 huajiri watu 20,105, na mapato yanatarajiwa kuongezeka kwa 4.7% kufikia mwisho wa mwaka 2014, kutokana na ongezeko la ushindani wa eneo la kuzika na ndivyo  idadi ya watu wanaotaka kuchomwa inaongezeka.

Kukiwa na soko kubwa na lenye faida kubwa, haishangazi kuona makampuni ya teknolojia yamekuwa yakitolea macho huduma za mazishi.

Usia wa Video
Usia wako wa mwisho, kwa mfano ni programu tumishi ya iphone "app" inayomruhusu yoyote kuweka ujumbe wa mwisho kwa wapendwa wao kwa njia ya "usia wa video" ambao utaonekana wakishafariki dunia.

Unatengeneza na kupakua video binafsi yenye usia na halafu unakuwa na neno lako la siri QR code – Ni bar code inayosomeka kwenye simu za kisasa – ambayo humpa mtu unayemwamini unayehisi atakuwa hai utakapofariki.

Ukishafariki dunia, mtu huyo uliyemwamini atatia saini kwenye programu tumishi kwa kutumia alama hiyo ya siri na atapata barua pepe itakayokuwa na ujumbe wako wa mwisho. Baada ya hapo ujumbe huo utatumwa moja kwa moja kwa watu wote uliowakusudia.

Kampuni hii inakiri kuwa "katika nchi nyingi, usia kupitia video haiwezi kuwa mbadala wa usia wa maandishi”, lakini kwa malipo ya ziada, Usia wako wa mwisho unatoa fursa kwa video yako kutumika kisheria kwa kile kinachoitwa ”mchakato mwepesi”.

"Kifo bila shaka ni jambo la huzuni lakini halikwepeki katika maisha ya mwanadamu na ni rahisi zaidi kuacha ujumbe wa mwisho au usia kupitia video kuliko njia iliyozoeleka, inayomhusisha mwanasheria na mashahidi,” Wolfgang Gobler, mkurgenzi mkuu na muasisi wa Usia Wako, aliiambia BBC.

Anaamini teknolojia itaendelea kushawishi huduma za mazishi Uingereza na dunaini kote.

"Kutakuwa na biashara nyingi zinazohusiana na mazishi siku za usoni. Nimeshakutana na wengine ambao ndio kwanza wanaanza huduma hizo za maisha na vifo," amesema.

Chanzo: BBC.
Imetafsiriwa na Mwandishi wetu

No comments:

Post a Comment