Sunday, 28 September 2014

DENNIS KIMETTO WA KENYA AVUNJA REKODI, BERLIN

Dennis Kimetto

Dennis Kimetto wa Kenya amevunja rekodi ya dunia ya mashindano ya marathon mjini Berlin, akishinda katika kipindi cha saa mbili, dakika mbili na sekunde 57.

Kimetto mwenye umri wa miaka 30 alichomoka kwenye kundi la watu saba wakiwemo wenzake kutoka Kenya Emmanuel Mutai na Geoffrey Kamworor. 

Alifanikiwa kumkimbia Mutai ikiwa zimebaki maili tatu tu na kuwa mtu wa kwanza kushinda marathon chini ya saa mbili na dakika tatu.

"Najisikia vizuri kwasababu nimeshinda katika mchuano mzito sana," alisema Kimetto.

"Nilikuwa najisikia vizuri tangu mwanzo na maili chache za mwisho nilihisi naweza na nitavunja rekodi."

No comments:

Post a Comment