Wednesday, 22 October 2014
'APIGWA MAWE HADI KUFA' NA AL-SHABAB
Mahakama ya kiislamu imempiga mawe hadi kufa kijana mmoja, kusini mwa Somalia baada ya kumkuta na hatia ya kubaka mwanamke mmoja, mtandao mmoja umeripoti.
Jaji aliamuru Hassan Ahmad Ali, mwenye umri wa miaka 18, kumlipa fidia ya ng’ombe mwanamke huyo kabla ya kuuawa, kulingana na ripoti moja ya redio iliyotolewa ya kuhusu hiyo.
Ali alikana kumbaka mwanamke huyo mwenye umri wa miaka 28, Fadumo Hasan Mohmoud.
Kundi la wapiganaji la al-Shabab linatekeleza sheria kali za kiislamu katika maeneo wanayoyadhibiti.
Mwezi uliopita, mwanamke mmoja alipigwa mawe hadi kufa katika mji wa bandari wa Barawe baada ya mahakama ya kiislamu kumkuta na hatia ya kuwa na waume wanne kwa mpigo.
Ali alikutwa na hatia ya kumbaka Bi Mohmoud huku akiwa kamshikilia bunduki katika kijiji cha Dharuro kwenye eneo la Shabelle, imeripoti kituo cha redio cha al-Furqan kinachoungwa mkono na al-Shabab.
Labels:
Habari
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment