Showing posts with label Video. Show all posts
Showing posts with label Video. Show all posts

Friday, 5 June 2020

Ushawahi Kubaguliwa? 'Zoom na Zoo' yajadili hayo



Gumzo katika 'Zoom na Zoo'. Kutokana na ghasia zinazoendelea nchini Marekani baada dunia 

kushuhudia namna George Floyd alivyouawa na polisi kufuatia kukamatwa na kukandamizwa 

shingoni hadi pumzi zikakata, mjadala kuhusu ubaguzi wa rangi umeibuka tena. Zuhura Yunus 

kazungumza na Dan Nkurlu akiwa Marekani, Najma Said -Ujerumani, Muhammed Omar- Uingereza 

na Salim Kikeke- Uingereza. wakieleza uhalisia wa ubaguzi.



Friday, 27 March 2015

FILAMU KUHUSU ALBINO YAZINDULIWA LONDON

   
 Katika miaka ya hivi karibuni, kumekuwa na ongezeko kubwa la mauaji ya albino, hasa katika mataifa ya Malawi, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo, Tanzania na vile vile Burundi. Watu hao hulengwa kutokana na itikadi za kichawi kwa madai kuwa viungo vyao huleta utajiri, bahati na kuponyesha maradhi yoyote. Filamu moja inayoangazia mauaji ya albino Tanzania 'White Shadow' imezinduliwa London wiki hii, Zuhura Yunus wa BBC alihudhuria uzinduzi huo.

Wednesday, 11 February 2015

VIBONZO VYARAHISISHA HISABATI KWA WATOTO TZ

    
Hisibati na Sayansi ni masomo yasiowavutia sana watoto, lakini Tanzania mtazamo huo unabadilika. Ubongo kids ni vibonzo vya elimu burudani,ya kwanza kwa Tanzania, inayofundisha watoto hisabati na sayansi kwa njia ya wanyama wanaoimba. Kipindi kinatazamwa na zaidi ya watoto milioni moja. Mwandishi wa BBC Tulanana Bohela anasimulia.

Monday, 12 January 2015

ANGA NAYO KUTUMIKA KAMA SULUHU YA FOLENI DAR?

     
Foleni ya magari katika miji mingi barani Afrika ni jambo la kawaida, na linalolalamikiwa kila mara. Kumekuwa na jitihada mbalimbali kujaribu kukabiliana na hali hiyo. Abiria pia wanatafuta njia zao kujaribu kuepuka foleni. Salim Kikeke ametembelea Dar es Salaam, na kushuhudia tatizo hilo, na suluhu inayotafutwa

Wednesday, 3 December 2014

MAHOJIANO YA BBC KUHUSU HIV 'KUPUNGUA MAKALI'

     
Utafiti mkubwa wa kisayansi umesema virusi vya HIV vinapungua makali kadri muda unavyoenda. Watafiti kutoka chuo kikuu cha Oxford wamegundua hilo baada ya kuwachunguza mamia ya wanawake nchini Botswana.
Kufahamu zaidi , Jo-Angeline Kalambo, mtaalam wa afya ya jamii katika shirika la Global Fund linaloshughulikia ukimwi, malaria na kifua kikuu, alihojiwa na BBC Dira TV mwanzo akitoa maoni yake kuhusu utafiti huo.

Monday, 1 December 2014

HOTELI CHINI YA BAHARI KISIWANI PEMBA, TANZANIA

   
Ushawahi kufikiria kulala na samaki? Au kuzungukwa na samaki. Hoteli ya kwanza chini ya maji barani Afrika imefunguliwa kisiwani Pemba nchini Tanzania. Hoteli hiyo ina umbali wa mita 250 kutoka baharini. Salim Kikeke katika matangazo ya BBC Dira ya Dunia anasimulia akiwa kisiwani humo.

Wednesday, 26 November 2014

ZITTO AHOJIWA NA BBC KUHUSU KASHFA YA ESCROW


 
Kashfa ya TegetaEscrow inazidi kufukuta nchini Tanzania. Mbunge wa Kigoma Kaskazini (CHADEMA) pamoja na Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) leo aliwasilisha ripoti ya uchunguzi katika bunge la nchi hiyo. Katika matangazo ya Dira ya Dunia TV, Zuhura Yunus alimhoji mbunge huyo kujua zaidi.

Wednesday, 17 September 2014

UFAHAMU ZAIDI KUHUSU KURA YA MAONI YA USKOCHI

Alhamsi wananchi wa Uskochi watapiga kura ya maoni kuamua iwapo wajitenge na Uingereza au la. Wananchi watajua ikiwa Uskochi itajiondoa kutoka muungano na Uingereza, muungano ambao umedumu kwa miaka 307.

Hadi sasa kura ya maoni inaonyesha kuwa kuna ushindani mkubwa kati ya wanaotaka muungano kuvunjwa na wale wanaotaka muungano kusalia.

Peter Musembi kutoka Idhaa ya Kiswahili ya BBC anakufahamisha zaidi

Thursday, 4 September 2014

UVUVI WA BARUTI TANZANIA

Ni biashara inayoleta kipato kikubwa, mamilioni ya dola kwa mwaka. Karibu asilimia kumi ya watanzania wanajihusisha na sekta ya uvuvi, kwa njia moja au nyingine, na kwa kutumia njia halali. Huku kukiwa na fedha nyingi, sekta hiyo inamulikwa pia na njia haramu. Moja wapo ni uvuvi wa kutumia baruti, katika kupata samaki kwa njia rahisi. Jambo hilo haliathiri uchumi pekee, bali pia mazingira.Salim Kikeke kutoka BBC ameandaa taarifa hii.

Wednesday, 3 September 2014

MWANAMKE WA KWANZA KUTANGAZA BBC DIRA YA DUNIA TV

Mtangazaji wa BBC Idhaa ya Kiswahili Zuhura Yunus amekuwa mwanamke wa kwanza kutangaza kipindi cha BBC Dira ya Dunia Tv kinachorusha matangazo yake kutoka jijini London.

Kipindi cha Dira ya Dunia ya BBC kilianzishwa miaka miwili iliyopita na watazamaji wake wakizoea kutazama sura za watangazaji wa kiume kama Salim Kikeke, Charles Hillary, Peter Musembi na Kassim Kayira .

 Lakini, Septemba 1, 2014, Zuhura Yunus alitangaza kwa mara ya kwanza kwenye kipindi hicho maarufu Afrika Mashariki na wazungumzaji wa Kiswahili duniani kote.

Bi Yunus ambaye ni mtangazaji wa BBC Swahili kwa muda mrefu sasa, ameungana na wafanyakazi wenzake kurusha matangazo ya Dira ya Dunia.

Hongera Bi Zuhura Yunus.

Chanzo: taarifa.co.tz