Tuesday, 9 June 2020

Ongezeko kubwa la vifo Nigeria lahusishwa na Covid-19



Vifo vingi Kano vilitokea nyumbani



Waziri wa Afya wa Nigeria Osagie Ehanire amesema 60% ya takriban vifo 1000 visivyoelezeka katika jimbo la kaskazini la Kano huenda vilitokana na Covid-19.

Kundi moja la utafiti lilikubaliana hivyo baada ya kufanya uchunguzi wa ongezeko kubwa la vifo katika jimbo la Kano mwezi Aprili na mapema mwezi Mei- hasa miongoni mwa wazee ambao walikuwa na magonjwa mengine hatarishi.

Baadhi walifariki dunia hospitalini lakini zaidi ya nusu walikufa nyumbani.

Kumekuwa na vifo vengine vingi kama hivyo visivyoelezeka katika majimbo mengine kaskazini mwa Nigeria.

Watu wachache wakiendelea kupimwa katika nchi yenye idadi kubwa ya watu barani Afrika, wataalamu wanahofia virusi hivyo vinaweza vikawa vinasambaa bila kutambuliwa Nigeria.

Mpaka sasa idadi ya watu wenye virusi vya corona vilivyothibitishwa ni 2,801 na vifo 361.

Chanzo:BBC

No comments:

Post a Comment