Thursday 4 June 2020

Covid-19: Watafiti Kenya watambua ‘aina tofauti’ za virusi

Getty images


Watafiti Kenya wametambua takriban aina tofauti tisa za virusi vya Covid-19 vilivyosambaa nchini humo katika jitihada za kufuatilia kubadilika kwa virusi hivyo.

Aina hizo 9 hazina tofauti na zile ambazo zimesambaa duniani kote.

Kundi la wanasayansi limetathmini mfumo wa jeni 122 kutoka kwa wagonjwa wenye dalili zilizo dhahiri na kwa wale ambao hazionyeshi licha ya kuwa wameathirika katika mji mkuu, Nairobi, na mjini Mombasa.

"Utafiti huo unaonyesha kuwa maambukizi yaliyogunduliwa na kuthibitishwa Machi 2020 zaidi ni kuwa virusi hivyo vimetokana na watu kutoka nje ya nchi, “ imesema ripoti hiyo iliyotolewa na Taasisi ya Utafiti wa Tiba Kenya (Kemri)

Sampuli zote zilichukuliwa kwa watu nchini Kenya baina ya tarehe 12 Machi hadi Mei 25.

Chanzo: BBC

No comments:

Post a Comment