Showing posts with label Burudani. Show all posts
Showing posts with label Burudani. Show all posts

Wednesday, 11 March 2015

WATUNZI WA BLURRED WAILIPA FAMILIA YA MARVIN GAYE $7m

Pharrell Williams and Robin Thicke perform at the Grammy Awards - 25 January 2015
Kibao hicho kilipata zaidi ya $5m kwa ajili ya Pharrell Williams (kushoto) na Robin Thicke

Baraza la wazee Marekani limetoa uamuzi kuwa walioandika wimbo wa Blurred Lines – miongoni mwa wimbo uliovuma na kuuzwa kwa wingi duniani – ulinakiliwa kutoka kibao cha Marvin Gaye.

Baraza hilo liliamua kibao hicho cha mwaka 2013 cha Pharrell Williams na Robin Thicke kilikiuka hatimiliki ya kibao cha Gaye cha mwaka 1977 kiitwacho Got To Give It Up.

Familia ya mwimbaji huyo wa miondoko ya Soul ambaye sasa ni marehemu imepewa dola milioni 7.3 za usumbufu.

Nona Gaye, daughter of Marvin
Mmoja wa binti zake Marvin Gaye Nona

Thicke na Williams walikana kunakili kibao hicho, na wakili wao alisema uamuzi huo unaonyesha “uamuzi mbaya sana”.

Wakati huohuo, wakili wa familia ya Gaye aliiambia Rolling Stone kuwa walitaka kuzuia uuzwaji wa wimbo huo wa Blurred Lines.

Gaye alifariki dunia Aprili 1984, akiwaachia watoto wake hakimiliki ya muziki wake.

Watoto wake - Nona, Frankie na Marvin Gaye III – walimshatki Thicke na Williams mwaka  2013.

                                                                           

Friday, 27 February 2015

GAUNI LA LUPITA NYONG'O LA $150,000 LAIBIWA



 

Gauni rasmi lenye thamani ya $150,000 lililoshonwa rasmi na kampuni ya Calvin Klein, na kuvaliwa na muigizaji Lupita Nyong'o wakati wa tuzo za Oscars, limeibiwa Hollywood.

Gauni hilo, lililopambwa na lulu nyeupe 6,000, liliibiwa katika hoteli moja, Nyong'o alipokuwa nje ya chumba chake.

Mkenya huyo alishinda muigizaji msaidizi bora mwaka jana kutokana na filamu ya Twelve Years a Slave na alikuwa miongoni mwa watangazaji katika shughuli ya Jumapili.

Jarida la People limemtaja kuwa mtu mrembo duniani wa mwaka 2014.

Polisi Lt William Nash alisema gauni hilo linaonekana kuibiwa siku ya Jumatano jioni na maafisa wanachunguza kupitia kamera za CCTV.

Hakuna aliyekamatwa mpaka sasa.                   

Calvin Klein ambaye ni mbunifu wa mavazi hajasema lolote kuhusiana na tukio hilo.

Chanzo: BBC
Imetafsiriwa na Mwandishi wetu

Sunday, 15 February 2015

LADY JAYDEE AFUNGUKA, AVUNJA NDOA NA GADNER

 

Mwanamuziki nyota wa kike nchini, Lady Jaydee jana aliamua kuwaburudisha mashabiki wake kwa staili ya kipekee; kuzungumzia kuvunjika kwa ndoa yake na Gadner Habash.

Kwa muda mrefu kumekuwa na minong’ono kuwa wawili hao wametengana, lakini hakuna aliyekuwa tayari kuweka wazi kuhusu suala hilo.

Hata hivyo, jana, Jaydee, ambaye jina lake halisi ni Judith Wambura aliamua kutoa ya moyoni, akisema kuwa kwa sasa ametengana rasmi na mtangazaji wa kituo cha redio cha E-fm cha jijini Dar es Salaam.

Jaydee ambaye wakati mwingine huitwa ‘Jide’, kwa wiki moja sasa ameamua kujibu maswali mbalimbali kutoka kwa mashabiki wake kwenye mitandao ya kijamii.

Kati ya maswali aliyoulizwa na mashabiki wake ni kama ni kweli ametengana na mumewe na ni sababu za kutengana.

Kupitia ukurasa wake wa instagram, mwanadada huyo alisema: “Nimemvumilia vya kutosha, kuhusiana na tabia zisizokuwa na nidhamu wala heshima ya ndoa na sasa imefika kikomo.”

Tuesday, 10 February 2015

BOBBI KRISTINA 'KUFA' SIKU MOJA NA WHITNEY




http://img2.timeinc.net/people/i/2013/news/130722/bobbi-kristina-600.jpg

Familia ya Bobbi Kristina Brown watachomoa mashine yake ya kupumulia siku ya Jumatano ili Brown aweze kufa siku ileile aliyokufa mama yake Whitney Houston, gazeti la New York Post limeripoti.

Bibi yake Brown na mama yake Whitney, Cissy Houston, alipendekeza wazo hilo mwishoni mwa juma, kulingana na the Post.

Familia inapanga kuchomoa mashine ya Brown ya kupumulia usiku wa Jumanne kuingia Jumatano.

Brown, mwenye umri wa miaka 21, amepooza tangu alipokutwa kwenye bafu nyumbani kwake huko Georgia, Januari 31.

Polisi wanafanya uchunguzi, wakimfutailia zaidi mpenzi wake Nick Gordon, aliyemkuta kwenye bafu hilo.

Inaripotiwa Brown alikuwa na majeraha usoni alipokutwa.

Whitney Houston alifariki dunia Februari 11, 2012, baada ya kuzama kwenye bafu lililojaa maji na baadae mwili wake ukikutwa na dawa za kulevya.

Familia yake na marafiki, akiwemo baba yake Bobbi Kristina, Bobby Brown, wameandaa sala ikiambatana na mishumaa siku ya Jumatatu huko Riverdale.




KANYE WEST ASEMA GRAMMYS 'HAZIHESHIMU SANAA'





Kanye West ameshutumu tuzo za Grammys kwa "kutoheshimu sanaa" baada ya kumpa ushindi Beck wa albamu bora ya mwaka badala ya Beyonce.

Alikuwa almanusra kuvamia jukwaa wakati Beck alipokuwa akitoa hotuba yake ya shukran.

Ilionekana kama West alikuwa arudie tukio alilofanya dhidi ya Taylor Swift, alipovamia jukwaa mwaka 2009.

Hatahivyo, alipohojiwa kwenye kipindi cha E, baadae alisema aliamua kutabasamu na kukaa chini baada ya kumfikiria binti yake.

 Msanii huyo wa miondoko ya hiphop alisema anaona Beck “angetakiwa kumpa Beyonce tuzo yake”.

"Ninachojua ni kuwa hizi tuzo za Grammys, kama wanataka wasanii wa kweli wawe wanarejea, wanatakiwa kuacha kutuchezea akili. Hatutoendelea kuzinguliwa nao." Alikiambia kipindi cha E, alipohojiwa akiwa na mkewe Kim Kardashian.

Sunday, 8 February 2015

BABA WA KIM KARDASHIAN APATA AJALI



Bruce Jenner

Polisi Los Angeles wamethibitisha nyota wa kipindi cha TV Bruce Jenner amehusika kwenye ajali iliyosababisha kifo cha mwanamke mmoja.

Jenner mwenyewe hakujeruhiwa, lakini wengine saba walipelekwa hospitalini.

Mwanamke mwenye umri wa miaka ya 70 alitangazwa kufariki dunia kwenye eneo la tukio huko Malibu.

Msemaji wa polisi wa LA alisema hapakuwa na dalili zozote kuwa Jenner, baba wa kambo wa Kim Kardashian, akifuatiliwa na mapaparazzi.

Msaidizi wa Jenner, Alan Nierob, alisema baba huyo mwenye umri wa miaka 65 hakuumia.

Sajeni Philip Brooks, kutoka iadara ya polisi ya Los Angeles, alisema gari aina ya Cadillac Escalade ya Bruce Jenner iliigonga kwa nyuma gari aina ya Lexus sedan, ambayo nayo ilikuwa imeigonga upande wa nyuma wa gari aina ya Toyota Prius.

Lexus hiyo ikaingia kwenye foleni iliyopo mstari mwengine na kugongana na gari jeusi aina ya Hummer.

Polisi walisema Jenner alishirikiana vyema na wachunguzi katika eneo la tukio na hakukutwa na pombe mwilini alipopimwa. Pia alipimwa damu.

Jenner alishinda dhahabu kwenye mashindano ya Olimpiki mwaka 1976 ya ‘decathlon’ lakini anajulikana zaidi kwenye kipindi maarufu cha TV Keeping Up With The Kardashians.