Sunday, 8 February 2015
BABA WA KIM KARDASHIAN APATA AJALI
Polisi Los Angeles wamethibitisha nyota wa kipindi cha TV Bruce Jenner amehusika kwenye ajali iliyosababisha kifo cha mwanamke mmoja.
Jenner mwenyewe hakujeruhiwa, lakini wengine saba walipelekwa hospitalini.
Mwanamke mwenye umri wa miaka ya 70 alitangazwa kufariki dunia kwenye eneo la tukio huko Malibu.
Msemaji wa polisi wa LA alisema hapakuwa na dalili zozote kuwa Jenner, baba wa kambo wa Kim Kardashian, akifuatiliwa na mapaparazzi.
Msaidizi wa Jenner, Alan Nierob, alisema baba huyo mwenye umri wa miaka 65 hakuumia.
Sajeni Philip Brooks, kutoka iadara ya polisi ya Los Angeles, alisema gari aina ya Cadillac Escalade ya Bruce Jenner iliigonga kwa nyuma gari aina ya Lexus sedan, ambayo nayo ilikuwa imeigonga upande wa nyuma wa gari aina ya Toyota Prius.
Lexus hiyo ikaingia kwenye foleni iliyopo mstari mwengine na kugongana na gari jeusi aina ya Hummer.
Polisi walisema Jenner alishirikiana vyema na wachunguzi katika eneo la tukio na hakukutwa na pombe mwilini alipopimwa. Pia alipimwa damu.
Jenner alishinda dhahabu kwenye mashindano ya Olimpiki mwaka 1976 ya ‘decathlon’ lakini anajulikana zaidi kwenye kipindi maarufu cha TV Keeping Up With The Kardashians.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment