Tuesday, 10 February 2015

WALIOBADILISHIWA WAZAZI UTOTONI WALIPWA

 

Wanawake wawili waliobadilishiwa watoto miaka 20 iliyopita wote wawili watapewa euro 400,000 euros ($451,760) kutokana na kosa hilo, kulingana na uamuzi wa mahakama moja kusini mwa Ufaransa.

Mahakama hiyo mjini Grasse nayo pia ilitoa amri kuwa zahanati hiyo binafsi iliyohusika na kuwachanganya watoto hao kulipa euro 300,000 kwa kila mmoja kwa wazazi watatu waliohusika, pamoja na euro 60,000 kwa kila kaka na dada walioathirika.

Mmoja miongoni mwa mama hao wawili aligundua kuwa mtoto wake si halisi baada ya kupima asidi nasaba mwaka 2004, miaka 10 baada ya binti huyo kuzaliwa.

Mabinti wote wawili walikuwa wakiumwa homa ya manjano walipozaliwa na kuwekwa kwewnye chombo kimoja cha kuhifadhi mtoto mjini Cannes.

Muuguzi aliwabidilisha watoto hao wakati wa kuwakabidhi mama zao. Wanawake hao walielezea wasiwasi wa kupewa watoto wasio wao wakati huo, lakini waliambiwa hakuna kosa lolote.

Chanzo: Reuters
Imetafsiriwa na mwandishi wetu

No comments:

Post a Comment