Majeshi ya Uganda yamekuwa yakimsaka LRA, Jamhuri ya Afrika ya Kati |
Jeshi la Uganda
limesema limegundua mabaki ya kamanda mwenye cheo kikubwa katika kundi la waasi
la LRA.
Okot Odhiambo alikuwa
mmoja wa makamanda watano waliopatikana na hatia katika mahakama ya uhalifu wa
kivita.
Inaaminiwa kuwa
kaburi lake limegunduliwa katika Jamhuri ya Afrika ya Kati.
Msemaji wa jeshi la
Uganda, Paddy Ankunda aliiambia BBC kuwa majeshi ya Marekani yalikuwa yakifanya
uchunguzi wa asidi nasaba (DNA) kujua iwapo ni mabaki ya mwili wa Bw Odhiambo
au la.
Kamanda mwengine wa
LRA, Dominic Ongwen, alifikishwa mahakama ya ICC wiki iliyopita.
Mkuu wa waasi hao,
Joseph Kony, bado hajulikani alipo.
Mkuu wa waasi hao, Joseph
Kony, bado hajulikani alipo.
No comments:
Post a Comment