Saturday, 7 February 2015
MBUNGE MUCHAI AUAWA KENYA
Mbunge wa Kenya na wasaidizi wake watatu wamepigwa risasi na kufa katika mji mkuu Nairobi, kwa kile ambacho polisi walielezea kama shambulio “lililopangwa vyema”.
George Muchai alikuwa akielekea nyumbani mjini Nairobi, ambapo ghafla gari lake likavamiwa na gari nyingine.
Bw Muchai, walinzi wawili na dereva wake walikufa hapo hapo.
Lengo la shambulio hilo, lililolaaniwa na rais pamoja na kiongozi wa upinzani, bado halijajulikana.
Polisi walisema washambuliaji hao waliiba mkoba na bunduki za walinzi.
Bw Muchai alikuwa mbunge kutoka chama tawala cha muungano Jubilee na alichaguliwa kwa mara ya kwanza miaka miwili iliyopita.
Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta alisema alishtushwa na shambulio hilo, akimwita Bw Muchai “mtumishi wa kweli wa watu”.
Kiongozi wa upinzani Raila Odinga naye pia amelaani mauaji hayo, lakini amesema ni sehemu pana zaidi ya ukosefu wa usalama Kenya.
Labels:
Habari
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment