Wednesday, 11 February 2015

MAKERERE KUCHUNGUZA 'SHAHADA BANDIA'


Makerere University in Uganda

Moja ya vyuo vikuu bora Uganda imeanza uchunguzi wa madai kuwa wanafunzi wamekuwa wakituzwa shahada bandia.  

Miongoni mwa wahitimu 12,000 kutoka chuo kikuu cha Makerere, takriban 600 hawakufikia viwango vinavyotakiwa, maafisa walisema.

Wanafunzi wote hao 600 wanaochunguzwa walikuwa wamehitimu masomo ya sayansi za jamii.

Makamu wa mkuu wa chuo Ernest Okello Ogwang aliiambia BBC kuwa alishuku matokeo ya mtihani yalibadilishwa kusudi.

William Tayeebwa, mkuu wa idara ya uandishi wa habari wa Makerere, aliiambia BBC kuwa mwanafunzi mmoja alifeli mtihani kwa 44%, mara matokeo yakabadilika na kuwa 71%.

Lakini wanafunzi saba kutoka idara ya uandishi wa habari ambao walikuwa na sifa zote na kuidhinishwa kuweza kuhitimu walikuja kugundua majina yao hayakuwepo katika orodha.

Bw Ogwang alikiri kuwa "huenda kuna udanganyifu". Alisema mashaka hayo ya udanganyifu unadhihirisha “udhaifu” katika mfumo wa chuo hicho ambapo “inabidi kuangaliwa kwa makini”.

1 comment:

  1. Tabia hii ya udanganyifu inahatarisha sana si sifa ya chuo tu bali hata ubora wa elimu na maendeleo ya taifa zima. Ni lazima tabia kama hizi zikemewe vikali

    ReplyDelete