Benki moja inayoshughulika na kusafirisha pesa kati ya Wasomali waishio Marekani kwenda kwa familia zao Afrika Mashariki inatarajiwa kufunga huduma zake kukiwa na wasiwasi kuwa fedha hizo hutumwa kwa wapiganaji.
Merchants Bank of California hushughulikia 80% ya huduma hizo kutoka Marekani, zenye thamani ya takriban dola milioni 200 kwa mwaka.
Lakini benki hiyo imesema haitoweza kuendelea kutoa huduma hiyo kutokana na utaratibu mpya ulioanzishwa wa ulanguzi wa fedha.
Mbunge mmoja wa Marekani aliielezea uamuzi huo kuwa na "athari kubwa”.
Wasimamizi wana wasiwasi kuwa baadhi ya fedha hizo zinazotumwa huenda zikaishia mikononi mwa wapiganaji wa kundi la al-Shabab.
Abdullahi Ismail, raia wa Marekani aliyezaliwa Somalia anayeishi California, aliiambia BBC kuwa jumuiya ya Wasomali imeshtushwa na uamuzi huo.
No comments:
Post a Comment