Thursday, 12 February 2015
WANAFUNZI WAISLAMU WAONGEZEKA MARADUFU ENGLAND NA WALES
Idadi ya watoto wa Kiislamu wanaohudhuria shuleni England na Wales karibu imeongezeka mara dufu tangu mwaka 2001, ripoti moja imesema.
Takwimu katika sensa ya mwaka 2011 inaonyesha mmoja kati ya wanafunzi 12 ni waislamu.
Idadi kamili ya Waislamu Uingereza imeongezeka kutoka milioni 1.55 mwaka 2001 hadi milioni 2.7 mwaka 2011.
Wakati chini ya nusu ya Waislamu Waingereza walizaliwa Uingereza, 73% hujitambulisha kama Waingereza.
Dr Sundas Ali, mchambuzi wa ripoti ya Baraza la Waislamu Uingereza, alisema “taarifa fupi na halisi” ya maisha ya Muislam.
Ripoti hiyo inasema idadi ya Waislam Waingereza imeongezeka haraka tangu mwaka 2001, huku theluthi ya idadi hiyo au chini yake wakiwa chini ya umri wa miaka 15 wakati wa sensa ya mwaka 2011.
Lakini inasema 46% ya Waislam Waingereza wanaishi katika maeneo maskini England – na kuongezeka tangu sensa ya mwaka 2001.
Mwandishi wa masuala ya dini wa BBC alisema hali ya kiuchumi iliyoelezwa kwenye ripoti hiyo “inachanganya” na wakati “Wengi wa Waislamu Waingereza wakiwa wafanyabiashara, takriban nusu wanaishi kwenye mazingira ya kimaskini mno”.
'Hali halisi ya kijamii'
Ripoti hiyo inasema 6% ya Waislam wanapata tabu kuzungumza Kiingereza, huku 24% walio na umri zaidi ya 16 wana sifa za kuchukua shahada, ukilinganisha na 27% ya idadi kamili ya watu wote.
Kulikuwa na wanafunzi Waislam wa shule za kutwa 329,694 mwaka 2011 - 43% wasichana na 57% wavulana.
Hatahivyo, imesema 71% ya Waislamu wanawake kati ya umri wa miaka 16 na 24 hawana ajira, ukilinganisha na takriban nusu ya idadi kamili ya watu wote.
Kwa wanawake kati ya umri wa miaka 25 hadi 49, inasema 57% ya Waislam wanawake wameajiriwa, ukilinganisha na 80% ya wanawake wote kwa jumla.
Chanzo:BBC
Imetafsiriwa na Mwandishi wetu
Labels:
Habari
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Mashaallah.
ReplyDelete