Sunday 8 February 2015

'KINYESI' CHA BINTIYE KUMWONGEZEA UZITO



Toilet paper

Mwanamke mmoja ameongezeka uzito kwa kiwango kikubwa baada ya kuhamishiwa bakteria kutoka kwenye kinyesi ‘stool transplant’ cha binti yake, madaktari walisema.

Ni utaratibu halali wa kitabibu kuhamishia bakteria wazuri kwenye utumbo ulioathirika, lakini madaktari wa Marekani wanahisi huenda imeathiri eneo la kiuno.

Ghafla aliongezeka kwa kilo 16 na sasahivi anachukuliwa kama mtu mwenye maradhi ya unene kupindukia.

Mtaalamu mmoja wa Uingereza alisema uhusiano baina ya bakteria wa tumboni na unene kupindukia bado hauko wazi.

Kuhamishiwa bacteria ‘wazuri’ wa kinyesi kwenye kiungo cha mtu mwengine hasa kwenye utumbo ‘faecal microbiota transplant’ – ambao baadhi huita "transpoosion" – kumeungwa mkono rasmi na huduma za kutoa afya za Uingereza mwaka jana.

Tiba mpya


Hutumika kwa watu ambao wameathirika sana kwenye utumbo na bacteria anayeitwa  Clostridium difficile

Hii inaweza kusababisha kutapika, kuharisha na maumivu ya tumbo na si mara zote unaweza kutibiwa na dawa za kupambana na vijidudu ‘antibiotics’.

Mwanamke huyo mwenye umri wa miaka 32, aliathirika kiasi ambacho hakuweza kupata tiba na hata dawa zenye nguvu sana.

Dr Colleen Kelly, kutoka chuo kikuu cha Udaktari cha Brown, alisema uwezekano wa kutumia tiba hiyo ya kuhamishiwa bakteria kutoka kwenye kinyesi kilijadiliwa na mwanamke huyo aliyetaka kutumia kinyesi cha ndugu – yaani binti yake.

Wakati huo utaratibu huo ulimponyesha mwanamke huyo.

Lakini Dr Kelly aliuambia mtandao wa BBC News: "Alikuja kama mwaka mmoja baadae na kulalamika kuongezeka uzito kupita kiasi.

"Alihisi kama kitu kimegeuka mwilini mwake – mpaka hii leo anaendelea kupata matatizo."

No comments:

Post a Comment