Monday, 2 February 2015

WATOROKA JELA WAKITUMIA MASHUKA, INDIA


 India police (file picture)

Zaidi ya wahalifu vijana 90 wametoroka kutoka kizuizini katika jimbo la Uttar Pradesh, kaskazini mwa India, polisi walisema.

Wahalifu hao, wote wakiwa chini ya umri wa miaka 18, walitoa vyuma vilivyopo kwenye dirisha na kufunga mashuka waliounganisha pamoja ambayo walitumia kushuka nayo.

Walitokea nyuma ya jengo mjini Meerut huku polisi wakiwa wamelinda kwa mbele.
Wafungwa thelathini na watano wamekamatwa mpaka sasa, polisi walisema.

Afisa mwanadamizi wa polisi Om Prakash ameliambia shirika la habari la AFP kwamba kutoroka huko kumefanywa  "kwa utaalamu mkubwa hata hamna aliyegutuka".

Kitendo hicho cha kutoroka kiligunduliwa baada ya baadhi ya wafungwa walipokutwa barabarani, wakijaribu kusimamisha magari mapema Jumatatu asubuhi.

Bw Prakash alisema wale ambao bado wamekimbia ni pamoja na wafungwa waliotiwa hatiani kwa uhalifu kama vile mauaji, ubakaji, wizi na ujambazi.

Zaidi ya wahalifu vijana 31,000  wanashikiliwa kwenye vituo maalum India.

No comments:

Post a Comment