Shirika la Fedha duniani IMF limekubali kutoa mkopo wa takriban dola milioni 700 nchini Kenya.
Fedha hizo zitatumika kama sera ya bima kujilinda kwa tishio lolote la uchumi wa nchi, ikizingatiwa nchi hiyo iko imara kiuchumi Afrika Mashariki.
Serikali ya Kenya iliomba pesa hizo kama njia ya tahadhari, iwapo kutatokea dharura kama vile majanga ya asili au mashambulio kutoka kwa wapiganaji.
Fedha hizo zitakuwepo kwa kipindi cha miezi 12 ijayo.
Wizara ya fedha imeiambia IMF haina nia ya kutumia pesa hizo.
Badala yake itatumika kama kinga dhidi ya “mtikisiko wa kiuchumi”, IMF ilisema.
Chanzo: BBC
Imetafsiriwa na Mwandishi wetu
No comments:
Post a Comment