Showing posts with label Michezo. Show all posts
Showing posts with label Michezo. Show all posts

Wednesday 11 February 2015

WASHINDI IVORY COAST WAMWAGIWA FEDHA


Ivorian President Alassane Ouattara and Ivory Coast captain Yaya Toure wave at the crowd

Timu ya mpira ya Ivory Coast imezawadiwa mamilioni ya dola na serikali ya nchi hiyo kwa kushinda Kombe la Mataifa ya Afrika.

Rais wa Ivory Coast Alassane Ouattara anampa kila mchezaji ambao jumla wako 23, nyumba yenye thamani ya dola 52,000 kila moja na pia pesa taslimu ya kiwango hicho hicho kwa kila mmoja, serikali hiyo ilisema.

Timu hiyo imeishinda Black Stars ya Ghana 9-8 kwa mikwaju wa penalti kwenye fainali ya shindano hilo Equatorial Guinea.

Shirikisho la Soka la nchi hiyo pia limepewa mamilioni ya fedha na wafanyakazi wengine wa timu hiyo.

Kwa jumla serikali hiyo imetoa zaidi ya dola milioni 3 kwa kusherehekea ushindi huo.
Timu ya Ghana nao hawakuachwa nyuma, licha ya kushindwa.

Kila mchezaji amepewa dola 25,000 na mfadhili wa timu hiyo, ambao ni shirika la mafuta la taifa Ghana (GNPC), kiwango ambacho waziri wa michezo wa Ghana ameona ni kidogo.


Monday 9 February 2015

IVORY COAST YASHINDA KOMBE LA AFRIKA 2015

Ivory Coast wameshinda taji la Kombe la Afrika mwaka 2015
Ivory Coast wameshinda taji la Kombe la Afrika mwaka 2015 kwa mikwaju 9 ya penati Ghana 8

Timu ya soka ya Ivory Coast imenyakuwa taji la Kombe la Afrika la mwaka 2015 kwa kuitandika timu ya Ghana kwa mikwaju ya penati.

Ivory Coast imeshinda kwa mikwaju 9 ya penati huku Ghana ikipata mikwaju 8.

Boubacar Barry, 35, ndiye aliyeibuka kidedea kwa kufunga penati ya mwisho baada ya mlinda mlango wa Ghana Razak Braimah kukosa penati.

Ghana walipata penati 8 huku Ivory Coast wakishinda kwa penati 9
Ghana walipata penati nane huku Ivory Coast wakishinda kwa penati tisa

Mlinda mlango mkongwe wa Ivory Boubacar Barry ndiye nyota wa mchezo wa leo.

Mashindano hayo yalikuwa yanafanyika nchini Equatorial Guinea.


Chanzo: taarifa.co.tz

Sunday 8 February 2015

MASHABIKI WA MPIRA WAZUA GHASIA, 14 WAFARIKI



 Egyptian firefighters extinguish fire from a vehicle outside a sports stadium in a Cairo"s northeast district

Takriban watu 14 wamefariki dunia katika mapambano yaliyozuka baina ya mashabiki wa mpira na polisi nje ya uwanja wa mpira mjini Cairo, chombo cha habari cha taifa cha Misri kimeripoti.

Mashabiki wa klabu ya mpira ya Zamalek walijaribu kuingia uwanjani kutazama mechi bila tiketi, na kuchochea ghasia hizo, maafisa walisema.

Vurugu hizo zilianza kabla ya mechi baina ya pande za Zamalek na ENPPI.

Februari 2012, zaidi ya watu 70 walikufa katika ghasia zilizozuka baada ya mechi huko Port Said.


Monday 19 January 2015

ASAMOAH GYAN KUCHEZA DHIDI YA SENEGAL?



 Asamoah Gyan

Kapteni wa Ghana Asamoah Gyan anaugua “malaria” na huenda asiweze kucheza dhidi ya Senegal siku ya Jumatatu.

Shirikisho la Mpira la Ghana lilisema mshambuliaji huyo alilazwa hospitalini huko Mongomo siku ya Jumamosi jioni na kutolewa Jumapili asubuhi.

Ugonjwa huo “uligunduliwa mapema” na Gyan anaendelea vizuri baada ya kupata matibabu.

Kiongozi wa timu ya Senegal Alain Giresse lazima aamue kuhusu afya ya Sadio Mane, ambaye amekuwa hachezi baada ya kujeruhiwa mguu.

Mchezaji huyo wa Southampton alijumuishwa kwenye timu hiyo licha ya klabu yake kusisitiza kuwa hatokuwa na afya nzuri ya kucheza.

Chanzo: BBC                                                

Friday 9 January 2015

YAYA TOURE: MCHEZAJI BORA AFRIKA





Kiungo wa Manchester City Yaya Toure amekuwa mchezaji wa kwanza kutajwa kuwa mshindi wa tuzo ya CAF  wa mchezaji bora wa Afrika kwa miaka minne mfululizo.

Toure, mwenye umri wa miaka 31, alitajwa kuwania tuzo hiyo baada ya kuchangia kwa kiasi kikubwa kushinda Ligi Kuu ya England na Kombe la Ligi.

Pia aliisaidia Ivory Coast kufuzu kucheza kwa Kombe la Mataifa ya Afrika 2015.

Toure ameweza kuwashinda mshambuliaji wa Gabon Pierre-Emerick Aubameyang na mlinda mlango wa Nigeria Vincent Enyeama.

Kiungo Toure alitajwa miongoni mwa wachezaji wa kuwania tuzo ya Ballon D’Or  2014 ya Fifa mwezi Oktoba.

Wednesday 7 January 2015

MUHAMMAD ALI ATOLEWA HOSPITALI


Muhammad Ali
Picha imepigwa 2006

Bondia wa mabondia Muhammad Ali ametolewa hospitalini baada ya kulazwa mwezi uliopita alipopatwa na maambukizi katika njia ya mkojo.

Aliyekuwa bingwa mara tatu wa uzani wa juu wa masumbwi duniani, amerejea nyumbani baada ya kutolewa siku ya Jumanne, msemaji wa familia alisema.

Bob Gunnell alisema Ali mwenye umri wa miaka 72 amepona kabisa na familia yake inamshukuru kila mmoja kwa sala zao.

Ali alitambuliwa kuwa na ugonjwa wa kutetemeka ‘Parkinsons’ mwaka 1984 baada ya kustaafu ndondi.

Alionekana hadharani mwezi Septemba, eneo alipokuzwa Louisville katika sherehe za kutoa  Tuzo za Kutetea Haki za Binadamu za Muhammad Ali.

Jina la hospitali ambapo Ali alitibiwa halijatolewa.

Chanzo:AP

Sunday 4 January 2015

SCHUMACHER AREJEA NYUMBANI

 

Michael Schumacher ameondoka hospitali ili kuendelea na matibabu akiwa nyumbani, lakini aliyekuwa mshindi wa mashindano ya mbio za magari ya langalanga Formula One anakabiliwa na "safari ngumu na ndefu siku za usoni" baada ya ajali mwaka jana, kulingana na meneja wake.

"Hivyo, kurejesha hali yake ya kawaida itafanyika nyumbani kwake. Ukizingatia majareha mazito aliyoyapata, kumekuwa na maendeleao mazuri katika kipindi cha wiki na miezi kadhaa," ilisema taarifa fupi iliyotolewa na meneja wake Sabine Kehm.

Msemaji wa hospitali ya chuo kikuu huko Lausanne amethibitisha kuwa Mjerumani huyo mwenye umri wa miaka 45, mshindi wa dunia mara saba, aliondoka.

Schumacher alipata majeraha makubwa ya kichwa baada ya kupata ajali kwenye mchezo wa utelezi wa barafu (skii) nchini Ufaransa mwezi Desemba na akahamishiwa Lausanne mwezi Juni baada ya kuibuka kufuatia kupooza.

Alipatiwa matibabu kurejesha hisia zake.

Chanzo: Al-Jazeera
Imetafsiriwa na Mwandishi wetu

Sunday 21 December 2014

MUHAMMAD ALI APELEKWA HOSPITALI



Muhammad Ali, pictured at a celebrity boxing match in 2012
Ali, aliyepigwa picha hii mwaka 2012, amekuwa na maradhi ya kutetemeka 'Parkinsons' kwa miaka 30 

Aliyekuwa bingwa mara tatu wa uzani wa juu wa masumbwi amepelekwa hospitali akiumwa mapafu ‘pneumonia’, msemaji wake alisema.

Ali, ambaye ana maradhi ya kutetemeka ‘Parkinson’, yuko katika hali nzuri, Bob Gunnell ameviambia vyombo vya habari.

"Uchunguzi unaonekana kuwa mzuri," Bw Gunnell alisema, akiongeza kuwa kukaa kwa mwanandondi huyo mwenye umri wa miaka 72 hospitalini kutakuwa kwa muda mfupi.

Hakutoa taarifa nyingine ya ziada na kutaka ombli la familia ya Ali kuachwa bila kubughudhiwa iheshimiwe.

Ali alipatikana na ugonjwa huo wa kutetemeka mwaka 1984, miaka mitatu baada ya kustaafu ndondi.

Alionekana hadharani katika sherehe mwezi Septemba, eneo alipokuzwa huko Louisville kwa ajili ya Tuzo za kusaidia Binadamu za Muhammad Ali.