Sunday, 4 January 2015

SCHUMACHER AREJEA NYUMBANI

 

Michael Schumacher ameondoka hospitali ili kuendelea na matibabu akiwa nyumbani, lakini aliyekuwa mshindi wa mashindano ya mbio za magari ya langalanga Formula One anakabiliwa na "safari ngumu na ndefu siku za usoni" baada ya ajali mwaka jana, kulingana na meneja wake.

"Hivyo, kurejesha hali yake ya kawaida itafanyika nyumbani kwake. Ukizingatia majareha mazito aliyoyapata, kumekuwa na maendeleao mazuri katika kipindi cha wiki na miezi kadhaa," ilisema taarifa fupi iliyotolewa na meneja wake Sabine Kehm.

Msemaji wa hospitali ya chuo kikuu huko Lausanne amethibitisha kuwa Mjerumani huyo mwenye umri wa miaka 45, mshindi wa dunia mara saba, aliondoka.

Schumacher alipata majeraha makubwa ya kichwa baada ya kupata ajali kwenye mchezo wa utelezi wa barafu (skii) nchini Ufaransa mwezi Desemba na akahamishiwa Lausanne mwezi Juni baada ya kuibuka kufuatia kupooza.

Alipatiwa matibabu kurejesha hisia zake.

Chanzo: Al-Jazeera
Imetafsiriwa na Mwandishi wetu

No comments:

Post a Comment